Ijumaa, 10 Februari 2017

الاستاذ هد هد(kuhusu VALENTINE DAY) NAUISLAM

. HISTORIA YA SHEREHE ZA SIKU YA VALENTINE

  

   Asili yake ni sherehe ya kipagani iliyoanzia mjini Rome Italy.Ikaingia kuwa ya kidini na sasa imekuwa ikitumika kama ni msimu wa kufanya biashara huria ambapo biashara za vyakula na mapambo ya maua, dhahabu na vyakula kama chakleti huchangamka sana.

  Warumi wa kale walisherehekea siku za tarehe 13,14 na 15 kwa matambiko mbali mbali yenye lengo la kutafuta uzazi kwa jina la siku ya Lupercalia.Wanyama wa kila aina walichinjwa ambapo vijana wa kiume walijitapakaza damu zao na kubeba mikia ya wanyama hao huku wakiwa uchi na kufukuzana na wasichana huku wakiwapiga migongoni kwa lengo na kukuza urutuba wa uzazi.Warumi hao waliamini kuwa muasisi wa mji wa Rome anayeitwa Romulus siku moja alinyonyeshwa na mbwa mwitu na ndipo akawa mwenye hekima na shujaa.

  Ukristo ulipoingia Rome pole pole sherehe hizi ziliingia ndani ya mafundisho ya dini.Kwa mfano yapo masimulizi kwamba Valentine alikuwa ni kasisi (bishop) mnamo mwaka 197 A.D wa mji wa Interamna ujulikanao sasa kama Terni.Kasisi huyo aliuliwa na viongozi wa kijamii baada muda mfupi kutokana na imani yake ya kikristo.Inaaminika alikufa siku ya Februari 14.

  Kisa kingine kinamtaja kasisi mwengine wa mji wa Rome kwa jina la Valentine ambaye naye inaaminika aliuwawa Februari 14.Kosa lake la mwanzo linatajwa kwamba  akiwa jela aliweza kumponya upofu  motto wa afisa gereza ambaye baadaye akafanya mahusiano naye ya kimapenzi.Alikuwa akiandikiana barua naye kwa kutumia damu yake kama wino.Hiyo barua ikiweka saini yake kama  “From your Valentine”.Kisa kingine cha kufungwa kwake inasemekana mtawala wa Rome wa wakati huo Claudius alikuwa amekataza wavulana kuoa ili awe na askari wazuri.Kasisi Valentine aligundulika kufungisha ndoa kwa siri ikabidi akamatwe.

   Mnamo mwaka 496 A.D papa wa wakati huo Gelasius kwa kuvutiwa na wimbi la sherehe za siku ya Valentine akaamua kwamba kila Februari 14 iwe ni siku ya sherehe ya kikristo kwa ajili ya kumuadhimisha St.Valentine.

   Kuifanya Februari 14 kama siku ya wapendanao kulipata nguvu zaidi mwaka 1382 wakati  Richard П wa London alipotangaza uchumba na Anne wa Bohemia.Richard aliandika   “For this was on St. Valentine's Day/ When every fowl cometh there to choose his mate.”.

   Mwaka 1400 A.D mahakama maalum ilifunguliwa  siku ya Valentine kushughulika na kesi mbali za mambo ya mapenzi kuhusiana na wachumba kupigana,kuachana na mateso mengine ya kimapenzi.

 Kufikia mwaka 1601 sherehe za Valentine zilikuwa zimezoeleka sana katika maisha ya kawaida kiasi kwamba  William Shakespeare aliandika katika shairi lake

 “To-morrow is Saint Valentine's day,/All in the morning betime,/And I a maid at your window,/To be your Valentine.”.

 

  

  Utaratibu wa  kutumiana kadi za mapenzi ulianza rasmi mwaka 1847 jijini London wakati shughuli za uchapishaji ziliporahisika.Mwaka 1929  kwa mara nyengine sherehe za Valentine zilileta janga kubwa pale magenge matano  jijini Chicago,Marekani  yalipopigana na kuuana kwa risasi  kuhusiana na mambo ya mapenzi.

    Katikati ya ya miaka ya 1980 makampuni  ya madini na biashara nyenginezo  yalianza kuziteka nyara sherehe za Valentine kwa  kuhamasisha  watu kununua bidhaa zao.

 

     Kutokana na historia hii itaonekana kwamba  sherehe zaValentine Day  hazina uhusiano wowote na uislamu.  Allaah سبحانه وتعالى   anasema:

((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))

((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]

 Mtume  صلى الله عليه وآله وسلمametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى  katika desturi na mila zao kama ifuatavyo:

((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم

((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni