Ijumaa, 27 Januari 2017

Mwanafunz mchawi 7

Mwanafunz mchawi 7

Ilipo ishia

.....DOREEN alimkubalia Eddy kuwa mpenzi wake lakini alimweleza kuwa kuna sharti ambalo Eddy lazima alifuate ndipo awe nae.Dorice hakutaka kukubali kirahisi kumwachia Doreen kuwa na Eddy hivyo alipanga kulipiza ili Doreen asije kumsahau.Mwalimu John alipigwa na mkewe mpaka akapoteza fahamu ambapo mkewe alichanganyikiwa sana baada ya kumwamsha bila mafanikio....

Endelea.....

...MWALIMU JOHN alikuwa kimya pale kitini akiwa hana fahamu yoyote, mkewe akazidi kuchanganyikiwa sana kwani alihisi tayari mumewe ameaga dunia.

"Jamani mume wangu amka bado nakupenda! Nisamehe Mimi John wangu!" Alizidi kulia mke wa mwalimu John kwa huzuni na majuto makali. Alijiona mjinga sana kwa kujichukulia maamuzi mkononi bila hata kumdadisi vizuri.

Simanzi ilimtanda mwanamke yule bila kujua la kufanya, machozi yalichuruzika kama mito miwili usoni kwake kwani ndio kwanza ndoa yao ilikuwa changa kabisa tangu waoane miezi mitano iliyopita sasa iweje John aage mapema kiasi hicho? Mkewe aliufikiria upweke ambao angekabiliana nao Siku za usoni. Huzuni ikamzidia.

Mwalimu John akiwa bado ameyafumba macho yake akahisi yumo kwenye usingizi mzito sana lakini alikisikia vyema kilio cha mkewe.

Alitamani aamke ili amtulize mkewe lakini mwili ulikuwa kama umegandishwa na sumaku. Hakuweza hata kutikisika, ghafla akahisi upepo mkali sana ndani ya nyumba yake alipotazama ukutani akakutana na sura ya kutisha sana.

Huku ikifuka moshi mdomoni, macho mekundu kama damu na kichwani yalichomoza mapembe mawili marefu. John aliogogopa sana kwani tangu azaliwe hakuwahi kukutana na kiumbe wa ajabu na wakutisha namna ile. Alitamani azinduke usingizini lakini hakuweza, hivyo alibaki akitetemeka.

Ghafla kiumbe yule akabadilika na kuwa sura ya msichana mrembo sana. Mwalimu John akabaki kinywa wazi akistaajabu ya Mussa. Alipotazama vizuri aligundua ni Doreen , akashtuka sana.Doreen alimtazama mwalimu John kwa dharau sana kisha akaachia kicheko kikali sana.

"Mimi ni Doreen Mbwana! Daima usinichezee maana sichezewi kirahisi.. Unataka kuniendea Malawi we? Hahahahah umechelewa sana John, nina nguvu kuliko unavofikiria"

Doreen akamsogelea John, na kutoa kucha zake ndefu nyembamba kama msumari kisha akamgusa mdomo John."Umeniita Nimekuja! Sasa utaipata fresh...! Hahahahahahahhh" alisema Doreen kisha akatoweka . John alihema kwa nguvu sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani maneno ya Doreen yalimtisha.

Mke wa Mwalimu John alizidi kulia baada ya kuona mumewe haamki kwa muda mrefu. Kelele Za kilio chake ziliwafikia majirani ambao walikuja kwa wingi kushuhudia kilichotokea. Bila hodi majirani hao walitiririka kama utitiri nyumbani kwa mwalimu John.

"Kuna nini jirani?" Aliuliza Mzee mmoja aliyejulikana kama Makorokocho.

"Hata sielewi mume wangu kapatwa na nini jamani...sielewi mimi" mke wa John alizidisha kilio.

"Kwani imekuaje?"

"Msogelee umwangalie maana mimi sielewi.. Namwita haamki.."

"Mh!" Aliguna Mzee Makorokocho huku akimsogelea mwalimu John.

Akamtikisatikisa John akamwita lakini John hakuitika, Ingawa John alisikia kila kitu kinachoendelea ila hakuweza kuamka.

"Mh! Mama pole sana huyu tayari ametangulia mbele za haki..."

"Ati mini?"

"Ndo ivo mama chamsingi tuwapigie ndugu zake simu, taratibu za mazishi zifanywe!"

"Hapana! Mume wangu hajafa! Iweje John afe mbele yangu.. Aaah we Mungu we!!" Mke wa Mwalimu John alilia kwa uchungu sana.

Ndugu wa mwalimu John wakapigiwa simu kupewa taarifa za msiba, taratibu za mazishi zikaanza kufanywa.

                                        *******

Dorice alipotoka bwenini kwao akaongoza moja kwa moja mpaka bweni la Mapambano ambalo ndilo alilokuwa akiishi Eddy, alitembea kama mwendawazimu mpaka alipotia timu katika bweni hill bila kujali ni bweni la wavulana pekee. Dorice aliongoza mpaka kitanda cha Eddy ambapo alimkuta Eddy akiwa na wenzake watatu. Na alikuwa akiwasimulia juu ya uhusiano wake mpya na Doreen.

"Habari zenu" alisalimia Dorice akiwa amevimba kama kiboko aliyekasirishwa. Eddy hakujibu isipokuwa wale rafiki sake.

"Umefuata nini hapa we mpuuzi?"

"Nimekufuata wewe nataka nijue kama unanipenda mimi au Doreen?"

"Hivi we mwanamke unawazimu we? Nikupende wewe kama nani? Doreen ndo mpenzi wangu, nampenda sana."

"Kweli!?"

"Ndio tena niondokee hapa, unanitia kinyaa!" Eddy alimsukuma Dorice kwanguvu Dorice akaanguka chini na kujigongesha kichwa kwenye kitanda.

"Eddy usifanye ivo bhana utamuumiza mwenzio" alisema rafiki mmoja wa Eddy kwani alimuonea huruma sana Dorice.

"Achana nae mpumbavu huyo"

"Lakini kumbuka mlikotoka"

"Achana na mimi kama unampenda si umchukue!"

Maneno Yale yaliziidi kumuumiza Dorice, aliinuka pale chini akajifuta vumbi maana bweni lilikuwa na vumbi kupita kiasi.

"Sawa Eddy! Daima kumbuka sio kila king'aacho ni dhahabu... Utanikumbuka!" Alisema Dorice kwa huzuni na kutoka.

"Akukumbuke nani wewe? We boya tu huna lolote" Eddy aliropoka maneno hayo huku akiwashangaza rafiki zake kwani daima hawakujua kama Eddy angemchukia Dorice kiasi kile kutokana na mapenzi yao yalivokuwa.

"Ama kweli watu wanabadilika..!" Alisema rafiki take Eddy na kuondoka zake.

Dorice aliondoka zake mpaka bwenini kwao, akachukua begi lake dogo na kuweka vitu vyake muhimu. Isipokuwa nguo za shule na madaftari, baada ya kupaki vizuri akachukua kanga akaivaa baada ya kutoa nguo kisha akaenda bafuni kuoga.

Alipooga na kujiandaa vizuri alikaa kitandani kwake huku kila Mara akitazama SAA yake ya mkononi ambayo alipewa na Eddy enzi za mapenzi yao. Ilikuwa SAA nzuri ya Dhahabu."Ikifika SAA kumi na mbili jioni lazima nitoroke ... Siwezi kubaki hapa!" Aliwaza Dorice akiwa kitandani kwake.

Muda huchelewa sana pale unapousubiri ndivyo ilivokuwa kwa Dorice. Muda ulichelewa lakini ukafika, kigiza kilipoanza tu akachukua begi lake na kutoka bwenini. Hakuvaa nguo za shule hivyo haikuwa rahisi kugundua kama ni mwanafunzi wa pale. Taratibu akazipiga hatua ili atoroke shuleni pale.

Licha ya kwamba alisumbuliwa na maswali ya wanafunzi wenzake ila hakujali ingawa aliwapa majibu ya uongo yanayoridhisha.

Shule ya mabango ilikuwa imezingirwa na miti mingi hivyo akapita katikati ya miti hiyo ili asioneakane kirahisi. Alipokuwa anaendelea kutembea ghafla akaona kitu mbele yake akashtuka.

                                        ********

Jioni ile tulivu Eddy na Doreen walikutana kwenye mti mmoja mzuri na tulivu. Walikuwa wamekumbatiana kimahaba huku wakipeana denda za kutosha.

"Baby nakupenda sana" alisema Eddy

"Nakupenda pia ila..."

"Ila nini mpenzi?"

"Sharti la kuwa na mimi ni kwamba hutuwezi kufanya mapenzi..." Alisema Doreen.

" eh! Kwanini?"

"Tukifanya hivyo kuna kitu kitatokea kwako?"

"Mh Doreen! Mbona sikuelewi, tutaishije kama wapenzi?"

"Nivumilie tu... Ila bado nina bikra"

"Nataka niitoe bikra yako Doreen please!"

" huwezi kufanya mapenzi na mimi, pia kuna sharti lingine mbali na hilo..."

"Bby hapa siwezi kuwa na wewe bila kufanya mapenzi, siwezi! Halafu pia siwezi kukuacha au huniamini?"

Alisema Eddy akiwa amezidiwa na hamu ya mapenzi na ilikuwa kazi ngumu sana kwake kujizuia....

Itaendelea ......

Mwanafunz mchawi 6

.mwana funz mchawi 6

Ilipo ishia

Eddy alimwacha Dorice Solemba, akilia na moyo nje ya darasa. Na alipoingia darasani Eddy alifuatwa na Doreen kwenye kiti chake, na alitaka kumwambia kitu muhimu....

Endelea...

Doreen alizidi kujilegeza sana kwa Eddy ili amteke kimawazo na kiakili sawasawa. Alirembua macho kama aliyekula kungu huku akimtazama Eddy.. Hakika kwa urembo aliokuwa nao Doreen na vituko alivofanya alizidi kuziteka hisia za Eddy haswa. 

Mtoto wa kiume alijikuta anaishiwa pozi, uvumilivu ukamshinda akajikuta anakohoa kidogo ili asafishe koo na kuweza kusema la moyoni.
 

"Eddy!" Doreen aliita kwa sauti ya mvuto sana.

"Naam"

"niambie basi.."

"ah!.. Doreen kama nilivosema awali wewe in mzuri sana hivyo basi .... nataka uwe mpenzi wangu.. please! naomba unielewe!" Eddy aliongea kwa sauti ya chini ili majirani wasiweze kusikia.

"Eddy! we ni shemeji yangu siwezi kumsaliti rafiki yangu Dorice!" Doreen alijifanya kukataa ingawa moyoni mwake alifurahia ushindi wa kumpata Eddy ilhali warembo wore shuleni pale waliikosa nafasi ile isipokuwa Dorice.

"Doreen! plz naomba nikubalie nakupenda sana "

"Na Dorice je?"

"habari za Dorice achana nazo me nimeachana nae, nakupenda wewe"

"mi sitaki Eddy!" sauti aliyoitoa Doreen ilionesha kabisa alikuwa anataka Ila alivunga tu.

"Nikubalie Dori.. nakupenda Doreen.. usinitese!" Eddy alisema huku machozi yakimlengalenga kwani hakutaka kumkosa Doreen. Ama kweli dawa za Doreen alizotafuna kabla ya kumfuata Eddy zilifanya kazi vizuri sana.

"Okey! nakubali kuwa na wewe!"

"Oh my God kweli Doreen unanipenda? asante sana!" Eddy aliachia tabasamu mwanana na alitamani hata kumkumbatia Ila aliogopa kufanya vile kwani walikuwa darasani.

"Nakupenda Eddy Ila kuna sharti moja muhimu inabidi ufate ili uwe na Mimi..."

"sharti gani tena?" Eddy alishtuka

"upo tayari?"

"ehm.. ah ndio coz I love u.. ntafanya"

"good.. nafurahi sana"

"Niambie basi mpenzi.." alisema Eddy akitabasamu.

"usijali nitakuambia baadae..."

Alisema Doreen huku akiinuka kitini na kuondoka zake. Eddy alikuwa na furaha sana hakuweza hata kusoma zaidi ya kumfikiria Doreen na kila Mara aliachia tabasamu.

Ilikuwa ni mchana majira ya SAA nane na nusu ambapo kengele iligongwa katika shule ya sekondari Mabango ambapo iliwaataarifu wanafunzi wote kuwa muda wa vipindi umekwisha na ni muda wa kupata chakula cha mchana.

Lakini haikuwa hivyo kwani wanafunzi walitakiwa waende mstarini ambapo Habari za kusikitisha sana zilipenya mioyoni mwa wanafunzi wote wa shule ile.

"Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi ameaga dunia Leo asubuhi kwa kifo cha ghafla kilichompata ofisini kwake..pia walimu wawili wana hali mbaya na wamefikishwa hospitalini kwa matibabu!" ilikuwa sauti ya masikitiko sana kutoka kwa Mwalimu Gallus iliyoonesha simanzi nzito sana aliyokuwa nayo.

Mwalimu huyo alishusha pumzi ndefu sana na kuendelea " Maombi yenu in muhimu sana kwa walimu wenu ambao wapo hospitali... na..." mwalimu Gallus alishindwa kuendelea kuzungumza kwani machozi yalikosa adabu yakashuka kwa kasi hivyo akaamua kuondoka eneo lile.

Wanafunzi wote waliondoka lakini mwishoni alibaki Eddy alitembea taratibu huku picha ya msichana katili anayejifanya mwema, Doreen ikizidi kumjia akilini mwake na kumfanya aisahau kabisa njaa aliokuwa nayo. Njia nzima alkuwa akizungumza peke yake kama mwehu mpaka alipofika bwenini.
 

"Ah Doreen! ni msichana mzuri sana! siamini kama amekuwa wangu..!" Aliwaza Eddy huku akiachia tabasamu kisha akabadili nguo na kujitupa kitandani. 

Alionekana kutoguswa kabisa na msiba wa mwalimu mkuu kwani tayari alikuwa amechanganyikiwa na Doreen. Hakumkumbuka tena Dorice ambaye kila Mara alimuahidi kutomsaliti kwa namna yoyote.

*******

Dorice alikuwa amekaa kitandani kwake huku machozi yakitiririka mashavuni mwake. Weupe wa ngozi ya USO wake ulibadilika na kuwa mwekundu kutokana na kulia kwa muda mrefu, hakuamini kama Eddy angemtenda kiasi kiasi kwani siku zote aliamini Eddy ndiye MTU pekee wa kumuamini, aliamini kama Eddy ndio furaha pekee ya moyo wake iweje Leo amtupe kama taka ya msafiri ndani  ya basi pale airushapo kupitia dirisha bila kujua itakapotua? Alimuona Eddy kama mnyama katili asiyekuwa na moyo wa utu.

Marafiki zake Dorice walizidi kumbembeleza atulie bila mafanikio yoyote.

"Kwa alichonifanyia Doreen, siwezi kumwacha kilahisi tu... lazima nimfanyie kitu..." Alijiapiza Dorice
 

" Ni lazima atajuta mpaka kifo chake... hatokaa anisahau kwa ntakachomfanyia.. lazima aelewe kuwa Mimi ni Dorice mtoto wa Kinyaturu sinyang'anywi tonge mdomoni kwa urahisi!" Alizidi kujiapiza Dorice akiwa amejifunika blanket mpaka usoni. Lakini baada ya muda mfupi Dorice aliinuka kitandani pale na kujifuta machozi kisha akapiga hatua za haraka kuelekea nje.

********

Mke wa Mwalimu John amuijia Juu Mumewe akitaka kujua suruali ile imetoka wapi. Lakini mwalimu John hakutaka kuweka wazi kile kilichomkumba shuleni.. alitaka iwe siri yake mpaka atakapofanikiwa kwenda Malawi kutafuta waganga wakumroga aliyemfanyia uchuro.
 

"John! umefumaniwa huko sio?" alifoka mke wa John

"usipaniki mke wangu tulia.. sijafumaniwa mim!" alijitetea mwalimu John bila mafanikio na wakati huo tayari mkewe alishaanza kumtandika makofi mumewe na alipoona haitoshi akanyanyua upawa na kumtandika nao Mwalimu John kichwani.
 

Ghafla John akanyong'onyea na kutulia kimya kitini bila kutikisika..

"John! John!" aliita mke wa mwlm John bila mafanikio John hakuweza kuitikia.

"Mime wangu... John wangu" alizidi kuita lakinu John alikuwa kimya, mkewe alichanganyikiwa sana.............

Itaendelea ......

Mwanafunz mchawi 5

.mwanafunz mchawi 5

Ilipo ishia

hivi we demu unajisoma??" alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
"Eddy! sijakuelewa!"
" unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?" maneno ya Eddy yalimfanya Dorice .....
 

SEHEMU YA 5
...DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy.
"we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?" aliuliza Eddy kwa ukali.
"Sijui" alijibu Dorice kwa huzuni
" Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu...." kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake.
"Eddy umesemaje?!" aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice.
" Hujanisikia? tena ukome kunifuatilia, usahau kama nilishakuwa mpenzi wako , unifute akilini mwako, sikupendi?" alisema Eddy akiwa amenuna kama aliyekula ndimu.
"unasemaje Eddy! hebu rudia nisikie"
"Sikutaki , sikupendi na sikuhitaji!" alisema Eddy huku akiondoka
"Eddy! Eddy! nimekukosea nini mpenzi wangu?"
"Achana na Mimi Dorice! huna hadhi ya kuwa na mimi , demu mwenyewe huna hata mvuto!" alisema Eddy na kusonya. Kisha akaenda zake darasani.
Alimwacha Dorice kwenye bahari ya simanzi na machozi yasiyoweza kuzuilika. Alilia kwa uchungu kama MTU aliyefiwa na MTU muhimu, lakini kilio hicho cha Dorice kilikuwa shangwe na furaha kwa Doreen. Alijiona kama mshindi kwa kufanikiwa kulivuruga penzi la Eddy na Dorice bila hata huruma kwani wawili hao walipendana sana na walikuwa na malengo makubwa katika maisha ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa pindi watakapotimiza malengo yao.

Doreen alicheka kwa dharau kisha akaondoka zake na kwenda darasani, ambapo alimfuata Eddy pale alipokuwa amekaa.
Eddy alimkaribisha Doreen kwa tabasamu mwanana na macho ya matamanio.
"Mambo Eddy handsome" alisema Doreen kwa sauti ya utulivu iliyomkuna vyema Eddy hadi akakosa ujasiri wa kuongea.
"Eddy mbona huitikii salam yangu?"
"Niko poa... vipi wewe mtoto mzuri"
"mh! nani mzuri Eddy?" Doreen alijifanya kuona aibu. Na kwakuwa darasa lilikuwa na kelele nyingi walipata mwanya wa kuzungumza zaidi.
"mzuri wewe hapo mtoto wa kitanga!"
"Acha hizo Eddy! mzuri no Dorice!"
"Eh! usinitajie huo uchafu"
"mh! uchafu tena? "
"ndio... Doreen bora umekuja hapa kukaa.. nina kitu muhimu sana nataka nikwambie"
"mh! kitu gani Eddy?" aliuliza Doreen huku akirembua jicho lake kubwa zuri kwa madaha.

***
Karatasi lile lenye ujumbe mzito lilitua mikononi mwa mtaaluma wa shule, kwa haraka macho yake yalitua kwenye maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi ile lakini maandishi yalikuwa tofauti na yale aliyoyasoma makamu mkuu wa shule, yalisomeka hivi "TOENI HUO MZOGA LA SIVYO MTAISHA"
Mwalimu yule wa taaluma aliogopa sana akashindwa kuongea akampasia karatasi mwalimu wa nidhamu lakini alipochukua tu ujumbe ulibadilika ukasomeka hivi "WEWE UTAMFUATA MAKAMU WA SHULE MAANA ULINITESA"

"ati nin? nilikutesa wapi Mimi? hata sio Mimi ujumbe haunihusu!" mwalimu wa nidhamu aliongea kwa kuchanganyikiwa na kwa hofu kubwa. Akampasia karatasi mwalimu mwingine lakini pindi anapompa mwalimu yule karatasi ujumbe ulibadilika tena "MNANISUMBUA! UKIMPA MWINGINE UJUMBE HUU UNAKUFA MUDA HUU.. NA UKINIWEKA CHINI UTAONA CHA MTEMA KUNI"
Mwalimu yule aliyefahamika kwa jina la mwalimu Jason alivuta pumzi ndefu sana huku mapigo ya moyo yakibadili mwendokasi na kwenda haraka sana. Akabaki ameshikilia karatasi lile mkononi mwake bila kuelewa cha kufanya .
WAlimu waliokuwa wanasubiri kusoma karatasi lile walimfokea mwalimu Jason kwa kuendelea kulishikilia karatasi lile kabla ya wao kulisoma.
"we vipi tupe na sisi tusome!"
"shukuru hamjasoma"
"Nini? usituzingue tupe hilo karatasi tusome bhana"
walimu walizidi kung'ang'ania karatasi lile lakini mwalimu Jason hakuwa tayari kuwapa ili kulinda uhai wake. Mwalimu Jasoni akaangalia upenyo ili aweze kutoka ofisini mle kisha akatoka mbio akiwa ameshikilia karatasi lake.

Mwalimu wa taaluma akaangalia pale chini ulipokuwepo mzoga wa Mbeshi akaona jinsi funza wallivyokuwa wakitapakaa kwa kasi.
"Jamani tumtoeni huyu tutakufa wote"alisema mtaaluma.
wakati huo makamu mkuu wa shule alikuwa akitokwa na haja ndogo kutokana na hofu ya kifo kama alivyoambiwa kwenye ujumbe.

***

Mwalimu John alionekana mwenye sana pindi aliporudi nyumbani kutokana na kitendo cha kudhalilika shuleni. Mkewe aliingia sebuleni na kumsogelea mwalimu John
"mume wangu vipi?"
"kwani vipi mke wangu?"
"nakuona hauna raha kulikoni?"
"nipo sawa... Ila... nina safari..!"
"kha! safari ya wapi tena mume wangu?"
"Naenda Malawi... Leo!"
"Malawi? kufanya nini mume wangu?"
"usijali kuna kazi muhimu naenda kufanya.."
"mbona ghafla sana? halafu mbona umevaa suruali ambayo si yako? au umefumaniwa?"
Aliuliza mke wa mwalimu john huku akimkagua mume wake kwa kupitisha macho kuanzia juu had I chin... ...

Itaendelea ......

Wanafunzi mchawi 4

Mwana funzi mchawi 4

Ilipo ishia sehem ya 3

)

 Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?" 
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."
 

 Sehemu ya nne

.... DORICE alishtuka sana kusikia Eddy ni mume mtarajiwa wa Doreen hakutaka kuyaamini maneno ya Doreen hata kidogo.

"hivi we Doreen umechanganyikiwa au upo timamu?" Dorice aliropoka kwa hasira.

 

" nikuulize wewe, hivi upo timamu au mwendawazimu unavomng'ang'ania mpenzi wangu Eddy? mpaka watu wanakushangaa! inaniuma sana Dorice usione nimekukaushia!" Alisema Doreen kwa msisitizo wa hali ya juu. Maneno ambayo yalizidi kumuumiza Dorice mpaka machozi yakaanza kumlengalenga machoni mwake. Alimtazama Doreen kwa hasira huku akiumanisha meno yake kwa ghadhabu, moyoni alitamani kumuadhibu vikali Doreen kwa kutaka kulitia DOA penzi lake na Eddy lakini hakuwa na uwezo huo.

 

"Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako! sitaki kuamini kama rafiki yangu kipenzi Leo unageuka adui yangu!"alisema Dorice huku akipiga hatua na kutaka kuondoka mbele ya mbaya wake. Lakini ghafla Doreen akamvuta shati na kumrudisha pale alipokuwa amesimama.

 

"we vipi? hebu niache niondoke?"

"nitakuachaje sasa wakati unaniharibia penzi langu na Eddy?" alisema Doreen kwa kujiamini sana huku akibetua midomo yake kwa dharau utadhani Eddy ni mpenzi wake kweli kumbe hakuna lolote ni tamaa na wivu vinavyomsumbua.

 

"umefanikiwa kuniumiza moyo wangu Doreen mpaka najuta kukufahamu.... haya Fanya lolote utakalo tena ili kunyang'anya haki yangu ya mapenzi... do it!" alisema Dorice kwa kwikwi kwani alishindwa kuzuia kilio chake kutokana na maumivu makali aliyoyapata moyoni mwake kwani maneno ya Doreen yalikuwa kama mkuki wenye sumu katikati ya moyo wake.

 

"hata Mimi najuta kukutana na mwanaharamu wewe, Kwa usalama wako achana na Eddy... sijui unanielewa?"

 

Dorice hakusema chochote zaidi ya kumkazia macho ya hasira Doreen, bila kujua kuwa kutazamana na Doreen kwa wakati ule ilikuwa ni kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe kwani Doreen aliitumia nafasi ile vizuri sana. 

Alijibadilisha macho yakawa ya kutisha sana kisha kila alipomtazama Dorice machoni alimhamishia vitu Fulani visivyoeleweka, kisha baada ya hapo Doreen alimsogelea Dorice na kumzodoa lakini haikuwa kumzodoa kwa kawaida Bali alimpaka vitu kama kamasi USO mzima na kumfanya Dorice atie kinyaa sana bila yeye mwenyewe kujitambua.

 

"hebu niondokee hapa mpuuzi wewe na ushukuru Mungu sijakufanya kitu kibaya" alisema Doreen baada ya kuhakikisha amekamilisha kazi yake aliyokusudia kwani sio siri Doreen alipania kumpata Eddy kwa vyovyote vile.

 

Dorice alitembea taratibu na kumfuata Eddy darasani huku akiendelea kulia.

Itaendelea........

Mwanafunz mchawi 3

MWANAFUNZI MCHAWI 3

Ilipo ishia sehem ya 2

. .Baada ya kukamilisha yote hayo Madam Mbeshi akasogeza kiti chake karibu na meza kisha akaketi halafu akaanza kusogeza vitu vilivyokuwepo mezani pale lakini ghafla akakutana na karatasi chafuchafu mezani kwake lakini ilikuwa na maandishi.

Akashtuka kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao....

 Sehemu ya tatu

...Mwalimu Mbeshi aliposoma ujumbe ule kutoka kwenye ile karatasi chafuchafu alizidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo yalimwenda kasi kama gari iliyokata breki ikiwa mlimani. akarudia tena na tena ujumbe ule uliosomeka "POLE SANA MWALIMU KWA MASWAHIBU YALIYOKUKUTA SHULENI KWAKO.. MIMI DOREEN MBWANA NIMEFANYA YOTE HAYO! PIA MUDA WA KIFO CHAKO U KARIBU KWANI UMESOMA UJUMBE WA MWANAFUNZI MCHAWI"

Jasho jembamba lilimtiririka mwanamama yule bila kuelewa afanye nini. Akataka kulitupa chini karatasi lile lakini ghafla akaona karatasi lile limebadilika ghafla, sio karatasi tena bali kitu kama ngozi ya binadamu iliyooza sana huku ikitoa harufu mbaya ikiwa imeambatana na funza wengi wakitembea tembea. 

Madam Mbeshi alihisi kinyaa sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani katika maisha yake hakuwahi kushuhudia mauzauza ya namna ile hats Mara moja. Alitamani akimbie lakini miguu ilikuwa imeganda kama msumari kwenye sumaku. 

Mbeshi alihangaika sana na wale funza mkononi mwake kwani walizidi kumpanda mwilini kwa kasi na kumtia ghasia. Machozi yalimtoka mwalimu mbeshi lakini kila tone lililodondoka lilikuwa damu. 

Hofu ikamzidia sana, hakuwa na tumaini la kusalimika tena kwani kwa hatua aliyofikia ilitisha sana. Na yote hayo yalisababishwa na binti Doreen Mbwana.

Ghafla mlango wa ofisi ya mwalimu Mbeshi uligongwa lakini Mbeshi hakuwa hata na uwezo wa kuzungumza chochote. Mlango uligongwa sana lakini Mbeshi hakuweza kuufungua ingawa alitamani yule aliyegonga mlango aingie ili iwe ahueni kwake lakini ilishindikana. 

Kila aliponyanyua kinywa ulimi ulikuwa mzito na hakuweza kuzungumza chochote ikambidi atulie kimya akiugulia mateso yake yalimzonga ndani ya muda mfupi tu.

"Masikini Mimi  inamaana ndo nakufa? masikini familia yangu ambayo Mimi ndio tegemezi! ee Mungu nisaidie!"aliwaza Mbeshi huku machozi ya damu yakizidi kutiririka.

                                    

 *******

Walimu hawakujua lolote linaloendelea ofisini kwa mkuu wa shule hivyo waliendelea na ratiba za shule kama kawaida.

Wanafunzi walienda mstarini, wakajipanga vizuri kwa mistari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha NNE.

Mwalimu John ambaye alikuwa zamu kwa wiki ile alikuwa amesimama mbele kwaajili ya matangazo lakini ghafla akasikia wanafunzi wachache wakimzomea. 

Moyo wake ukamlipuka akautazama msitu ule wa watu lakini macho yake yakatua moja kwa moja kwa wanafunzi wa kidato cha NNE, akamwona Dorice na nyuma yake alikuwa amesimama Doreen akiwa anacheka sana kwa sauti ya dharau na kiburi. Hasira za mwalimu John zikampanda akaumanisha meno yake kwa ghadhabu

"Doreen! hebu njoo mbele haraka sana!" alisema mwalimu John kwa sauti kali iliyojaa ghadhabu lakini bila aibu Doreen aliachia sonyo Kali iliyowafanya wanafunzi wote wamgeukie yeye na kumwangalia kwa mshangao.
"We mtoto! unanisonya Mimi? una adabu kweli?"
"Kwanini nisikudharau wakati we mwenyewe umejidharau?" alisema Doreen kwa kujiamini sana.
"Ati nini?"alishangaa mwalim John kwani hakutegemea kama Doreen angekuwa jeuri kiasi kile. 
"We unavokuja kazini hivo unategemea nini?"
"Vipi" alishtuka Mwalimu John.
"Unakuja kazini bila kuvaa suruali ili iweje!?" 
"Una wazimu wewe nani hajavaa suruali?"

"Jiangalie huko chini kama umevaa suruali;" alisema Doreen na kumfanya Mwalimu John ajiangalie vizuri akagundua kweli alikuwa hajavaa suruali. 

Alishtuka kupita kiasi wanafunzi wote wakamtazama Mwalimu John kwa mshangao kwani kweli alikuwa hajavaa suruali. Baadhi ya wanafunzi walicheka, lakini baadhi walimhuzunikia wakiamini kuna mchezo kachezewa na si bure.

Mwalimu John akakimbia mstarini pale Kama mwendawazimu na kwenda ofisini lakini kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu zake alikumbuka kuwa alipotoka nyumbani alikuwa amevaa suruali tena suruali yake mpya ya kadeti.

 "Sasa imeenda wapi?? mnh hapana kuna MTU kanichezea lazima nimweendee Malawi hata Nigeria ntafika Ila siwezi kumwacha" aliwaza Mwalimu John na wakati huo waiimu wenzake waliamua kwenda nyumbani na kumletea suruali nyingine ili aweze kuondoka Nayo.

 

********

Baada ya wanafunzi kuingia darasani kwao. Doreen aliamua kumuita Dorice nje kwani alikuwa na mazungumzo nae mazito sana.Dorice alionekana kuogopa kwani wito ule haukuwa wakawaida, akasimama kwa hofu akimtazama Doreen 

"vipi mbona unaogopa, unaogopa nini?" alisema Doreen.
"siogopi kitu!"alijibu Dorice 
"basi nisogelee" 
Dorice akamsogelea Doreen kwa hatua chache.
"Jana ulikuwa na nani pale kwenye mti usiku?" aliuliza Doreen huku akiuchezesha mguu wake wa kulia chini na mkono mmoja akiwa kaushika kiunoni.
"hukuniona au?" aliuliza Dorice kwa mshangao.
"jibu swali!"
"OK! nilikuwa na Eddy"
"nani yako Eddy?" 
"Doreen unanitisha ujue?"
"kha! nakutisha nina mapembe hapa? nijibu swali langu"
"Eddy mpenzi wangu!"
"nimekupata sasa... tangu lini Eddy mpenzi wako hujui kama ni mume wangu mtarajiwa?"
"Ati nini....... Eddy ni. .."

 

Itaendelea ......

Mwanfunzi mchawi 2


MWANAFUNZ MCHAWI
2

Ilipo ishia sehem ya kwanza

.....Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke yake nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe....  

Sehemu ya pili

...DOREEN aliendelea kuongea maneno aliyoyajua mwenyewe akiwa bado yupo uchi wa mnyama nyuma ya bweni alilokuwa anaishi. 

Ghafla kipande kidogo cha karatasi nyeupe kikashuka mikononi mwake bila kuonekana kilikotokea. Doreen alicheka kwa sauti Kali ya kutisha sana kisha akalikazia macho karatasi lile, matone ya damu yaliangukia kwenye karatasi lile kutoka kwenye macho yaliyotisha sana ya Doreen kwani yalikuwa na rangi nyeusi halafu yakawa na umbile kama macho ya paka.
 

"Nenda mpaka ofisi ya mkuu wa shule ukamalize kazi." alisema Doreen akiwa amelinyanyua karatasi like kwa mkono wake wa kushoto. Karatasi likatoweka mkononi mwake na kupepea kwa nguvu kama vile limerushwa na upepo mkali.

Doreen alipomaliza kazi hiyo akasimama vizuri kama mwanajeshi aliyejipanga kwaajili ya gwaride kisha akainamisha kichwa chake chini akapotea eneo lile.

**********

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mabango walikuwa wanahofu kubwa sana kila wakikaa walifikiria kifo tu. Usingizi haukuwajia hata Mara moja hivyo usiku waliketi makundi makundi wakizungumza hili na lile.

Wakati huo Dorice rafiki kipenzi wa Doreen alikuwa amejitenga pembeni akizungumza na mpenzi wake aitwaye Eddy, kijana mtanashati, mzuri, mpole na akili nyingi sana darasani.Wasichana wengi shuleni pale walitamani kuwa nae lakini bahati ilimwangukia Dorice pekee.
 

"Eddy unajua naogopa sana.." ilikuwa sauti ya Dorice akiwa amemkumbatia Eddy kwani kigiza kile cha usiku kiliwaficha wasionekane hivyo wakajiachia.

"unaogopa nini Dorice mpenzi wangu?"

"Naogopa kufa!" binti Huyo wa kinyaturu, mrembo aliyeumbika aliongea kwa sauti ya madeko sana.

"siku zote nakwambia Dorice kama Mungu alipanga huwezi kupangua , mwanadamu asikutishe kwa lolote. Huyu anayeua wenzake naye IPO Siku yake tu!"

"Najua baby Ila hali inatisha"

"Tuzidi kuomba Mungu mpenzi wangu kila unalofanya muombe Mungu."

"Nakupenda "

"Nakupenda pia"

Wakati Eddy na Dorice wakiendelea kuzungumza maneno hayo, Doreen alikuwa nyuma ya mti waliosimama hivyo alisikia kila kitu. 

Roho ilimuuma sana kwani tangu alipohamia shuleni hapo alitokea kumpenda sana Eddy na alitamaniawe mpenzi wake kwani ndio chaguo la moyo wake lakini Dorice alikuwa kikwazo. .

Suala hilo lilimuumiza Doreen ndani kwa ndani. Akainuka pale kwenye mti na kupita katikati yao, akamwita Dorice pembeni.

"Dorice.. mimi nawahi kulala Ila kesho unione!"

"nikuone?"

"ndio kwani hujaelewa?" alijibu Doreen kwa ukali jambo lililomwachia maswali mengi Dorice. Lakini Doreen hakujali kitu akaondoka zake Ila moyoni alipanga jambo zito la kumfanyia Dorice siku ya kesho yake.

*********

Ilikuwa asubuhi tulivu sana majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ambapo mwalimu Dayana Mbeshi aliwahi ofisini kwake kama ilivyokuwa kawaida yake. 

Majengo ya ofisi yalimkaribisha kwa shangwe naye akaitikia ukaribisho huo kwa kufungua ofisi yake kisha akasogeza mapazia ya dirishani ili kuruhusu mwangaza wa jua changa uweze kupenyeza vizuri. 

Baada ya kukamilisha yote hayo Madam Mbeshi akasogeza kiti chake karibu na meza kisha akaketi halafu akaanza kusogeza vitu vilivyokuwepo mezani pale lakini ghafla akakutana na karatasi chafuchafu mezani kwake lakini ilikuwa na maandishi. 

Akashtuka kidogo halafu akaichukua ili aisome vizuri. Mwalimu Mbeshi hakutaka kuamini kile alichokiona, akataharuki kwa hofu na mshangao...............

Itaendelea....

Mwana funzi mchawi 1

. Wakati twa fuatilia simulizi ya mke wa face boock tufuatilie na hii ili tusikae kimya sana
👇👇👇👇👇👇
MWANAFUNZ MCHAWI


SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu.

Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na USO wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule

"vipi kulikoni?"
"hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu.
"what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake.

******
Wanafunzi wengi walionekana kuwa na hofu sana baada ya vifo visivotarajiwa kuzidi kutokea katika shule yao. Kila MTU aliwaza sana juu ya vifo vile huku kila mmoja akihisi zamu yake IPO karibu. Nyuso za huzuni ndizo zilizotawala kwa wanafunzi wote si wa kike wala wa kiume. Hakuna aliyetamani kulala wala kukaa mbali na kundi la watu kwani hofu iliwajaa mioyoni mwao, hawakuweza hata kusoma.

Lakini hali ilikuwa tofauti sana kwa binti Doreen ambaye alikuwa na wiki tu toka ahamie shuleni hapo. Alionekana kutoogopa chochote wala kuguswa na misiba ya wanafunzi wenzake. Kila Mara alionekana akiwa na furaha, hali hii iliwatisha wanafunzi wenzake na kuwafanya wawe na maswali mengi juu yake.

Doreen alikuwa msichana mrembo, sura yake nyembamba iliyopambwa na macho makubwa legevu, kope ndefu nyeusi tii, pua nyembamba iliyochongoka vyema na midomo mizuri yenye mvuto wa aina yake vilimfanya awe tishio kila kona kwani alikuwa ni mzuri kupindukia lakini Tabia ilikuwa tofauti na uzuri wake.

Wakati wanafunzi wengine wakiwalilia wenzao Doreen alikuwa amejitenga peke take nyuma ya bweni alilokuwa anakaa na kulikuwa na Giza totoro. Alikuwa uchi wa mnyama huku mikono yake ikiwa imeshikilia vitu fulani huku akitamka maneno ambayo aliyaelewa mwenyewe.... 

Itaendelea.......

Jumamosi, 21 Januari 2017

Mungu wangu hajaniacha 4

. MUNGU WANGU HAJA NIACHA
Sehem ya 4

Www.mrhudhud.blogspot.com

Ilikua ni usiku palipo kucha asubui nikashktuka hapo siku muona yeyote kat ya watu nnao wajua nikashuka kitandani nakusimama taratibu nikaanza kusogelea mlango wa wodi huku wagonjwa wengine kama watatu hivi wakiwa vitandani mwao nilipo toka nje ya word nikajihis mwepes Sana kama karatasi maana sikuweza kutembea Bali ni kukimbia tu nika zunguka maeneo kadhaa Mara nikaskia sauti ikiita@jumanne mwanangu@

Niliitambua ni Sauti ya mama nikageuka nakuitika @naaam@mama akani kumbatia kW mda kidogo huku machozi ya kimtoka akatamka kwa sauti ya chini akisema@MUNGU WANGU HAJA NIACHA@  kisha akaniuliza @unajiskiaje mwanagu@nikamjibu@vizuri mama ila njaa INA niuma@ Bas MWANANGU twende ndani uka sbiri nkakitaftie chakula@ hapo tuabrudi wodin na mama kila alipo taka kutoka kuni taftia chakula bas watu walio fahamian waliingia na kunijulia hali mda simref mamdogo make wa baba (mama yangu wakambo) akaingia na chakula  na mi sikua na kumbuka chochote kumhusu yeye  nikatizama chakula alicho leta ni wali na maharage. Kweli aliniweza maana ndo chaKula nnacho kipenda nikila bila kubakisha  nilikaa hospitality siku tatu nikiwa na jitambua siku ya NNE tuliruhusiwa nakuondoka nje ya hospitali mama MZAZ na mama wa kambo waliongea namama akataka niongozane nae had nyumbani tulipo fika nyumbani niliwakuta wa dogo zangu wawili nuru na yasini wakanipa pole hapo nika pata swali LA kumuuliza mama @hiv mama mimi hospitali nilipelekwa Lin na nilikua naumwa nin@swali hili lili mfanya mama kwa dakika kadha kisha  akaniambia @pumzika mwangu ule alaf jion ntakwambia@ ilipo fika jioni nili mkumbusha mama juu ya swali langu hapo akaanza kuni ambia
@mimi nikiwa nyumbani mama yako mdogo alikuja hakuingia ndani akanambia jumanne anaumwa nika muuliza nini tatizo akanambia homa bas nika mwambia ntaenda kumuona yeye akaondoka nikaanza kunawa nikijua waumwa homa ya kawaida wakati na nawa akaja bibi mama hamis wa mitunduruni yeye alikuja na hasira @mama Jumanne una Fanya nini @nikamjibu nimeambiwa Jumanne anaumwa na nawa niende sokoni nipitie na huko@bibi akajibubkwa hasira@naona ume mchoka kwanobmpumbavu nibora roho ya mwanao ikatie mikononi mwako wahi ospitali mwanao anakufa @ hapo Nili changanyikiwa nika jikuta mtandio wa kichwani nine jifunga kiunoni sia wahi tembea kichwa wazi lakin sikuwaza hilo nikaondoka mbio na kumuacha bib nikiwa nijiani watu walinishangaa lakin sijujali maneno ya bibi mama hamis yalijirudia kichwani mwangu huku moyoni nikijisemea  mwangu Jumanne ndo kafa au nin tatizo hapo nika jikuta natamka kwasauti @MUNGU WANGU NAKUOMBA USINIACHE @ dakika 20 nilifika hospitali sikuwaza ntakupataje nikasikia sautu ikiniita @mama Jumanne nihuku@ watu walio nifaham waliniita na kunielekeza word hadi kitanda uliopo hapo nili kukuta umesha kaka maaa macho ya megeuka na kua meupe wabibi waliopo hapo waliniusi @funga utumbo@hapo niliaminibkua ushakufa  sikujua machozi yalikua wapi hayakutoka sijui nilitamani nini mbele yangu ni kamuona jirani wa baba yako nika muuliza @mama neema kime mkuta mwangu@ akanivuta pembeni na kuanza kuniambia

Itaendelea sehem ya 5

Kwa ushauri au maoni

Email
Alhabiibhudhud@gmail.com

Au tembelea blog yangu

Www.mrhudhud.blogspot.com

Alhamisi, 19 Januari 2017

SIMULIZI (MUNGU WANGU HAJA NIACHA)

. SIMULIZI YA KUSISIMUA

((MUNGU WANGU HAJA NIACHA))
Sehem ya 3

Msimuliaji
Dr hud hud
Www.mrhudhud.blogspot.com

Tunaendelea na sehem ya 3

Maisha yangu kwa mama wakambo yalianza mwanzoni sikupata shida wala tabu yetote lakin ikifikia wakati nikaikumbuka filam y kitanzania ilio chezwa na wabongo miaka hiyi ilio kua na jina @mama wakambo si mama@
Kwani dhahir nilianza kuumiss upendo wa mama yangu ambae alinijali        . alinipenda na kuni thamin nilipo umwa alilia na kuhangaika
Wakati huu chakula changu kilikua chashida kwani nilipewa chakula peke yangu tena nilipo toka shule nakukuta wamekula bas nami nililazimika kutoka kula kes za udokozi nyingi nilipewa Mimi ilimradi niadhibiwe tu  shule niliazima kalamu na nilipo kosa wa kuni azima bas sikuandika somo lolote siku hiyo na adhabu ya mwalimu zinili husu  asubuhi niliosha viombo nika fagia nyumba hadi uani zamu ya usafi tena kwa ugauzi wa mama mdogo nilichelewa shule Mara kwamara kwakweli maisha nilio yaish kwa mama wakambo yalikua y mateso hasa sikutakiwa kushtaki kwa baba neno lolote  naye hakujua lolote kwani alitoka alfajir kwenda msikitini hakurud akapitiliza kazini na kurud sa tatu au NNE usiku hakupat muda wa kuongea na mi .
Sikupat nafasi yakwend hata kwa mama kumsalimu nika jikuta nalazimika kuya zoea maisha ya mama wakambo
Siku moja nilitoka shule majira ya SAA nane nanusu nilipo fika nyumbani nilikua na njaa ukizingatia Jana yake usiku sikula kwakua nili kua na kosa LA mchana ambapo niilikata kamba iliokua imeanikiwa nguo bahat mbaya BA's adhabu yake usiku sikula   nilipo fika nyumbani nikaimba chakula  mamadogo akanambia niende jikoni ni kachukue nikaenda jikoni nikakuta ugali nkapakua na mlenda wa bamia  mboga ambayo sikuipendaga sana nilipendaga sana mlenda wa kusaga lakin wabamia sikuupendaga sana      .sikua na ujanja wa kukataa kwa kuhofiamajibu na adhabu kutoka kwa mama asie na huruma   wakati na kula nikaliona sufuria likiwa limefunikwa vizuri akili za utoto zikanituma nifunue nilipo funua nikakutana na nyama ilio rostiwa vizur kwa haraka nika funika nakurud mahala pangu Mara hii tonge LA mlenda halikufika kinywani na hata nilipo fanikiwa kulitafuna nilipata shida kuliy meza ladha yote ilipotea kumbukumbu za kuuchukia mlenda wa bamia zika tawala kichwani mwangu Nika waza ni kwanini ndipo nika gundua ni kwakua nimeona nyama ghafla madogo akapita nikajikut bila kufikiri ni kantanyua kinywa changua na kusema @mamdogo naomba mchuzi@kisha nika tulia kusubiria majibu yamvua na adhabu lakin yeye alanitazama bila ya kusemaneno akachukua bakuli aka weka mchuzi na nyama moja kisha akaingia na bakuli ndani Mara akatoka akiwa ana changanya siku jiuliza kwanin aliingia nalo ndani naje alikua akichanganya nini nikicho waza tu Mimi ni utam wa nyama bakuli lika wekwa chini @haya kula haraka haraka kuna kazi zina kusubir@yalikua ni maneno yake kish akaondoka nami nikaanza kula dakika chache baada nikachukua nyama na kueka mdomoni nika anza kuinyonya mfano wa embe mshumaa muda kidigo kizungu zungu na maumivi ya kichwa ya kaanza kunitawala nikanyanyuka na kujitupa kitandani nikalala kifudi fudi dakika chache sikujitambua      ninapo kuja kujitambua ni usiku Nokia na drip ya maji mkono wangu wakushoto namuona mama yangua mzazia kiwa analia nilipo tizama lokation kwa makin nikagundua ni hospital nikakoha kidogo kwa saut hali ilo wafanya watu wote kusimama  hadi wagonjwa walio vitandani walinyanyuka niliskia sauti ikiniita @jumanne MWANANGU @
Niilitambua ni sauti ya mama yangu Mzazi nami nika itika naaam hapo nikaskia MGONJWA mmoja akitamka @mungu mkubwa Sikh yanne Leo ndo ana pata faham kama MTU alie fufuka @maneno hayo yali ustua ubongo wangu nikapoteza faham na sikujitambua tena

Itaendelea sehem ya 4

Je nini kiliendelea baada ya kupoteza aham je nini kilisababisha awepo hospitality siku NNE bila kiji tambua
Usikose sehem ya 4

Tembelea blog yangu

Www.mrhudhud.blogspot.com

Au tuma ujumbe kwa emali

Alhabiibhudhud@gmail.com

SIMULIZI (MUNGU WANGU HAJANIACHA)

. SIMULIZI YA KUSISIMU

(MUNGU WANGU HAJA NIACHA)
Sehem ya pilli

Dr hud hud

Www.mrhudhud.blogspot.com

Alhabiibhudhud@gmail.com.com

Usiku ule story iliishia pale pale ikabidi tuka lale hatimae asubuhi na mapema nikaamka nkajiandaa kwenda shule haikua mbali  na nyumbani  jioni yake nilitamani mama amalizie story lakini sikupenda kumuona maa akiwa analia machozi nili nyamaza mama alikua akifanya biashara ndogondo sokoni Nazo hazikua nafaida sana kias kwamba wakati mwingine tulilala njaa Siku moja nilimueleza mama kua inaitajika Pesa shuleni ya kumlipa mlinzi pia nami sina daftar za kutosha masomo yangu mama aliamua kuniagiza kwa baba kazini kwake lakin baba hakunipa kwakusema hana pesha hajauza chochote toka asubui hali hii ili muudhi mama Mara kwamara   kwakua baba haku nihudimia chochote sichakua malazi wala mahitaji ya shule   hatimae mama aliamua kwenda ustawi wajamii kushtaki baba aliitwa    alipo kuja akasema kua yeye hawezi kuni hudumia ningali lwa mama labda nikaish kwake ikabid ofis za serikali zifanye maamuzi kua kunzia wakati huo niende kuish kwa baba binafs nilifurahu sana maana nilitaman kua karibu na baba tukarudi nyumbilani mama akaniandaa na kuni fungashia nguo zangu kwenye Rambo lakin uso wa mama ulionyesha wazi kua hakupenda niende huko lakin tayar ni agizo LA serikali Hakua na jins  jioni yake niilienda kwababa hapa kua mbali sana  nilitembe a kiss cha nusu SAA hatimae nkafika nakupokelewa na mke wa baba Tatar kuyaanza maisha ya hapo lakini nilikimbuka kaul moja ya mama wakati ananiandaa alisema @sasa unaenda kuish kwa mama wakambo kua makin utundu hacha yule mama yako was kambo ana roho mbaya+ maneno hayo yalijirudia kichwani mwangu huku nikijisemea -huyu ndo mama wakambo mbona hana hat shida +akili nyingine ikanambia baba yupo haina shida

Itaendelea sehem ya 3

Je maisha ya jumannw kwa mama wakambo ya takuaje
Usikose sehem ya 3

By mtunzi

Dr hud hud

Email

Alhabiibhudhud@gmail.com

Jumapili, 15 Januari 2017

HADITH YAKU SISIMUA (MUNGUWANGU HAJANIACHA )

. SIMULIZI ya KUSISIMUA

MUNGU WANGU HAJANIACHA
Sehem ya kwanza

By dr hud hud

Alhabiibhudhud@gmail.com

Ikiwa ni nyakati za jioni nime kaa na wadogo zangu wawili nuru na yasini  wakati mama yangu pia akiwa amekaa  Katika kigoda kidogo  alisema @leo nataka niqasimulie iidogo maisha yangu mie na baba yenu*
Mi nilifurahi sana kwani nilitamani kuskia historia yanyuma ya baba yangu maana toka nakua nakupat akili wakati huo nikiwa darasa LA pili shule yamsingi unyankindi singida mjin
Nime jikuta nikiiishi na mama nahali baba akiwa anaish kwingine na na mke mwingine hivyo nilitaman kujua kwanini Mimi siishi na baba yangu kama walivyo wengine.  Nikatega  skio kwa makin kusikiliza na mama bila kusita alianza
@ baba yenu wakati ana nioa mimi alikua  na mke mwingine hivyo Mimi nikawa mke mdogo kweli baba yenu alikua muadilfu na hakuelemea upande mmoja alitulea sote kwa Umoja na mshkamano mwanzoni tulipendana na kutembeleana kama MTU na mke mwenzake japo maisha hayakua mazuri lakini tulijali ITU kuliko kitu kazi ya naba yenu ilikua ni umachinga wa viombo haikuleta mafanikio ila toka mimi nilipo olewa tu mafanikio yalianza kujitokeza nilimshauri mume wangu kuachana na kazi ya kutembea kwani Siku ipenda ili mchosha sana na badala yake afungue japo duka LA kuuza viombo hivyo badala ya kutembea kweli ushauri ulimfaa akafungua kaduka ladogo na taratiibu mafanikio yalianza hali hio ili mfanya anikumbuke kila wakati akinitaja kwasifa njema kila wakati heshma yangu na utii vilimfanya kua na amni mda wote wakati kwamke mkubwa haya hakuanayo muda simref toka nimeolewa nkapata ujauzito mumewangu akazidiaha upendo kwangu hali ambayo  ili muudh mmkubwa japo alikua anawatoto wawili lakin hakutaka Mimi nipendwe vile miezi Tisa ikatimia nika jifungua MTOTO wakiume ambae ni wewe Jumanne.. Mama aliongea kwa kuni point mimi nilifurahi kupata hadithi ya kuzaliwa kwangu nkatega tena akio na kuendelea kumsikiliza mama
@niilijifungua salama lakini mwangu aliumwa kila mara na alipo fikisha umri wa miaka miwili. Nilianza kupata yaabu ya kukuuguza nidhahir kua mke mwenzangu aliniendea kwa waganga ili nimpoteze MWANANGU lakin hakufanikiw japo niliteseka sana kila jioni ilipo ingia Nili muuguza MWANANGU hadi alipo fikisha umri wamiaka minne nikapata ujauzito mwingine nakujifungua MTOTO wakiume tena nikaamuita ramadhani Mara hii mke mwwnzangu alinichukia dhahie na  kunitamkia wazi Mara kwamara kua @we kazana kuzaa lakini hapa utaondoka tu
.
Maneno yaliniuma lakini sikukata tamaa  kwahuyu tena niliteseka zaidi  mwanagu alimwa kila Mara zaid yahapo ilipo fika usiku wa manane niliskia saut zaajabu zikisema @ukitaka maisha ya amani tupe mwanao
Sauti hizi zili nitisha kwakweli sikulala ndipo Sikumoja usiku mwangu akiwa   na umr wamwaka mmoja usiku nikiwa nimelala niliota watu walio valia manguo meupe wamekuja na kumchukua mwangu huku mi nikipiga kelele mwacheni mwangu mar nkashtuka usinguzin na kumkuta mwanagu analia nka muwahi na kumpa ziwa nikawa kimya kwa dakika chache Mara nkahis mwangu kesha lala maan haku akinyonya tena hali iio nitisha ni kua mwangu hatakama yuko usingizin maada ziwa langu liko mdomoni alinyonya kwa kushtukiza laki wakti huu alikua kimya nikaamka nae nakuwasha taa ndipo nikaanza Julia kwa uchungu baada ya kuhakikisha kua mwangu amekufaa

Story ilikatizwa na machozi wadogozangu walikua wamesha sinzia lakin Mimi nililia hata mama pia hadi nikaachana nastor ikabidi nianze kumbembeleza mama Kwanzaa.......

Itaendelea.........sehem ya pili

Alhamisi, 12 Januari 2017

SOMA HAPA

. . .HABARI NJEMA wagonjwa na wenye shida mbali mbali

Dr hud hud sasa yuko karibu nawe

Usikose
ku Tembelea blog yangu

Kwa mambo yanayo ihusu afya na uchambuzi

Chasimgi tembelea blog yangu

Google alaf andika

((Www.mrhudhud.blogspot.com))

My gmail

Alhabiibhudhud@gmail.com

Au jiunge na group langu LA what's upp LA afya

👇👇👇👇
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/25Ub2o8xeDeA3wtNCAPlzL

👆👆👆👆👆
Kwa maswali yoote yanayo husu afya

Au piga sim namba 0672930143

UCHAWI NI NIN

. UCHAWI

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, toleo la 3, neno ‘uchawi’ limefafanuliwa katika sehemu kuu mbili zifuatazo, Kwanza ni ‘ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe; au juju. Pili ni ‘vifaa vinavyotumika katika shughuli za kurogea’

Neno “mchawi’ limetafsiriwa kuwa ni mtu anayesadikiwa kuwa anaweza kuwadhuhuru watu kwa kuwaroga; mlozi, kahini. Wachawi mara nyingi hufanya kazi katika ulimwengu wa roho yaani ulimwengu ambao huwezi kuuona kwa macho ya kimwili.

Kwa mujibu wa Merriam-Webster dictionary neno “witchcraft” ambalo katika Kiswahili hutafsiriwa kama “uchawi” limetafsiriwa kama “magical things that are done by witches, or the use of magical powers obtained especially from evil spirits” kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili “uchawi” maana yake mambo ya kimiujiza yanayofanywa na wachawi”, maana ya pili, “matumizi ya nguvu za kiroho zilizochukuliwa toka kwa roho waovu”. Wengine wanatafsiri uchawi kama matumizi ya silaha za mashetani au nguvu za mashetani ili kusababisha madhara kwa watu.

Iyke Nathan Uzorma, Katika Kitabu chake kinachoitwa “Mkuu Wa Wachawi Sasa Ampokea Kristo” anaandika hivi; mchawi ni mwanadamu ambaye hupitia vitengo mbali mbali katika ufalme wa giza, ili atumiwe kuzidhihirisha nguvu zisizoonekana za Shetani katika Ulimwengu wa mwili. Kwa lugha nyingine mwanadamu yeyote ambaye hutumia nguvu au maarifa yasiyoonekana kudhuru, kuharibu, kudhibiti, kumiliki, au kupumbaza akili za mwanadamu mwenzake huyo ni mchawi.

Tofauti kati ya Ushirikinana Uchawi

Yapo mahusiano kati ya wachawi na waganga hasa waaguzi, wapiga bao na wanaosoma nyota na washirikina. Mwangalizi mkuu wa WAPO Mission International askofu Sylvester Gamanywa katika makala yake “ongezeko la hofu ya uchawi makanisani” iliyochapishwa katika mtandao wa gospelkitaa.co.tz anasema Kuna makundi mawili yenye kushughulika na uchawi.

a) Kundi la kwanza ni la “washirikina” yaani jamii ya watu wanaoamini mambo ya uchawi na mizimu. Hili ni la “washirikina” ambao ni wateja wa “waganga wa tunguri” wenye kudai kutoa kinga na tiba dhidi ya uchawi.

b) Kundi la pili, ni jamii ya “wachawi wenyewe” wenye ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe, au juju nk. Kimtazamo, “mchawi” ni tofauti na “mshirikina” kwa kuwa “mchawi” ni “bingwa wa kuloga” wengine; na “mshirikina” ni “mteja wa mganga” anayetafuta msaada wa kinga au tiba dhidi ya uchawi. Kivitengo vya kiitikadi, wachawi ndio “viongozi wa kiroho” katika uchawi; wakati “washirikina” wao ni “waumini wanaosalishwa kwenye ibada za kichawi”. Kibiblia, uchawi, uganga watunguri na ushirikina vyote ni idara moja ya uchawi na wahusika wote ni wafungwa wa majini na mizimu na majeshi ya pepo wachafu.

Makundi manne ya wachawi kulingana na walivyoingia katika uchawi

a) Kundi la kwanza, walioingia kwa kurithi, wapo watoto wengi wanao zaliwa kwenye familia ambazo kuna mambo ya uchawi, na wanaingizwa katika shughuli za uchawi tangu wakiwa matumboni mwa mama zao. Katika huduma yangu nimekutana na watoto wadogo kabisa wa mwaka mmoja, wengine hata miezi miwili tu wakiwa tayari ni wachawi. Si unakumbuka Yohana Mbatizaji alijazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake, kabla hajazaliwa, na katengwa kwa kusudi maalumu la Mungu katika dunia hii (Luka 1:15). Usishangae kusikia Shetani amemjaza mtoto mdogo aliyopo tumboni mwa mama yake roho ya uchawi kabla hajazaliwa na mara nyingi watoto hawa huwa umilikiwa na mapepo kwa kibali maalumu toka kwa wazazi wake

b) Kundi la pili, walioingia katika uchawi na watu wengine kwa kulazimishwa, wapo watoto wengi na watu wazima waliochukuliwa na kuingizwa katika uchawi na hata wanapotaka kutoka ni vigumu kwao. Namna wanavyoingizwa katika uchawi inatofautiana mtu na mtu, nimeshuhudia watoto wadogo wakiwa wameingizwa katika uchawi na watoto wenzao baada tu ya kupewa vyakula kama vile maandazi, pipi, biskuti na kadhalika. Wengine walijikuta tu wapo kwenye Ulimwengu mwingine bila kujua waliendaje na baadaye wanajikuta wanapewa maelekezo ya kazi, pamoja na kurishwa viapo vya kuto kutoa siri na utii pindi unapo agizwa katika kazi yoyote ile. Kundi hili hufanya shughuli za uchawi kwa kushurutishwa na wanapojaribu kutaka kutoka vitisho na mateso huzidishwa. Watu wa kundi hili wanafanya shughuli za uchawi kwa shingo upande. Tumekutana na watu wa mtindo huo mara nyingi katika huduma.

c) Kundi la tatu, walioingia kwa hiari yao wenyewe, lipo kundi kubwa la watu ambao wameingia katika uchawi kwa hiari yao wenyewe kabisa, katika mikoa ya Pwani ya bahari ya Hindi si ajabu kusikia wapo watu ambao wanakwenda kununua majini ya uchawi kwa lengo la kupambana na maadui zao. Lakini pia inasadikika wapo watumishi wa Mungu ambao walianza vizuri, lakini kwa sababu ya tamaa ya pesa, na nguvu za miujiza wanaamua kuzigeukia nguvu za uchawi.

d) Kundi la nne, walioingia bila kujua, aidha  na watu wengine, au walijiingiza wenyewe pasipo kujua wanaingia katika jamii ya wachawi na hawajui kama wanatumika katika shughuli za uchawi (blind witches), Nakumbuka tuliwahi kufanya huduma ya binti mmoja ambaye alikuwa anashiriki katika shughuli za uchawi bila ya yeye kujua, baadae akaanza kusumbuliwa na maumivu makali ya kichwa kwa sababu alihamia nyumba ya wana maombi kama mfanyakazi wa ndani, tulipoingia katika huduma na yeye tulishitushwa kusikia kuwa binti yule alikuwa mchawi pasipo yeye kujua, asante Yesu kwasababu alifunguliwa na kuwekwa huru. Siku kadhaa baada ya huduma, nilkaa na yule binti kumuuliza mambo mawili matatu yaliyojitokeza katika huduma. Yule binti akaniambia mara nyingi alikuwa akiota ndoto yupo na kundi kubwa la watu asio wafahamu, na huko anajiona ancheza ngoma mbali mbali, anapika na kula nyama na vyakula mbali mbali. Na anapoamka asubuhi anajikuta kashiba, tumbo limejaa kabasa. Alikuwa mchawi aliyeingizwa na ndugu zake wa karibu kabisa pasipo yeye mwenyewe kujua.

Photo of mr hud hud images

Photo mr hud hud 

Mr hud hud images

Jumanne, 10 Januari 2017

JIUNGE NAMI

. . .HABARI NJEMA wagonjwa na wenye shida mbali mbali

Dr hud hud sasa yuko karibu nawe

Usikose
ku Tembelea blog yangu

Kwa mambo yanayo ihusu afya na uchambuzi

Chasimgi tembelea blog yangu

Google alaf andika

((Www.mrhudhud.blogspot.com))

My gmail

Alhabiibhudhud@gmail.com

Au jiunge na group langu LA what's upp LA afya

👇👇👇👇
Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/25Ub2o8xeDeA3wtNCAPlzL

👆👆👆👆👆
Kwa maswali yoote yanayo husu afya

MFAHAM MR HUD HUD

. MFAHAM MR HUD HUD ((prff: doctor)

Amezaliwa mkoa wa singida mjini kata yx kindai (tanzania)mwaka 1991 tar 27 mwezi 1 kabila lake ni mnyaturu.shule ya msingi kuanzia stand 1 mpaka stnd 3 (shule ya msingi unyankindi singida mjini) na stnd 4hadi 7 shule yamsingi ndurumet arusha
Kidato cha kwanza hadi cha NNE mkoa wa morogoro sec

Chuo

University of health nirobi Kenya

Pia ninmtaalam wa anatomia na fisiologia
Ni member wa kampuni ya green world intanationali t lmtd wa livil 3

Amechukia elimu ya dini ya kiislam
Almadrasatu taufiq (mitunduruni singida mjin)

Uhuru Muslim (morogoro mjini )

Annujuum collage (singida mjini)masomo alio chukua

Qur an

Tafsir

Hadith

Ahkaami tajweed

Na fani ya da.wa katika tasisi ya almalidi Islamic in a national PR.s. morogoro

Kwa sasa ni privert doctor na ana hudumia vipimo ushaur na Tina Feisal natural pathic clinic

Cont:0672930143
           0684549105

Gmail www.doctahudhud@fecboock.com

Blog
Www.alhabiibhudhud.blogspot.com

Jumatatu, 9 Januari 2017

UGONJWA WA PUMU

.UGONJWA WA PUMU

Utangulizi 
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya 

kupitishia hewa (bronchioles tubes)hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa 

nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake. 

Makundi ya Pumu

Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili; 
Pumu ya ghafla (Acute asthma): Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika kati ya shambulizi moja na jingine.Pumu sugu (Chronic Asthma): Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu, njia za hewa huzidi kuwa nyembamba zaidi.

Aina za ugonjwa wa pumu 

Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni 1.Pumu inayobadilika (brittle asthma):Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ta ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili, ambazo ni 
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla(asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.2.Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na 

matumizi ya dawa kadhaa,zikiwemo vitanua njia za hewa(bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka, na anaweza kupoteza maisha. 3.Pumu 

inayosababishwa na mazoezi(Exercise Induced Asthma): Hali hii husababishwa na ufanyaji wa kupitiliza wa mazoezi ya viungo. Kwa kawaida wakati wa kufanya mazoezi mtu hupumua kwa kutumia pua na kupitia mdomoni. Hata hivyo wakati 

mwingine hutokea hewa aivutayo huingia ndani ikiwa haijapozwa vya kutosha puani na hivyo kusababisha ongezeko la mtiririko wa damu katika mishipa inayosambaza damu katika mirija ya kupitisha hewa. Hali hii husababisha kuvimba 

kwa kuta za mirija hiyo na muhusika kupata shambulizi la pumu. Aina hii ya pumu yaweza kudhibitiwa na dawa. Inashauriwa sana kwa watu wenye matatizo kama haya kupasha moto misuli kwa mazoezi mepesi (warming up)kabla 

ya kuanza mazoezi mazito na ya muda mrefu. 4.Pumu inayosababishwa na aina ya kazi afanyayo muhusika (Occupational Induced Asthma): Wakati fulani, mazingira ya kazi yanaweza kusababisha kutokea kwa pumu hata kwa baadhi ya wafanyakazi wasio na tatizo hili. Mara nyingi aina hii huweza kuwatokea watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya kutengeneza matairi, vigae, rangi, kemikali mbalimbali, mbolea, chuma, unga na mbao. 

Pumu husababishwa na nini? 

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha kutokea kwa pumu au yanayohusishwa na shambulizi lake. Mambo hayo ni pamoja na 
Matatizo ya kinasaba: Matatizo ya kinasaba yamehusishwa na kutokea kwa karibu asilimia 90 ya ugonjwa wa pumu hususani kipindi cha utoto.Uvutaji wa sigara au tumbaku kipindi cha ujauzito pia unahusishwa na kusababisha pumu kwa mtoto atakayezaliwa.Maendeleo ya kiuchumi: Ugonjwa wa pumu umeonekana sana kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ikilinganishwa na nchi zenye maendeleo na hali duni ya kiuchumi.Magonjwa ya mapafu kamabronchitisVyanzo vya mzio(allergens)kama vile vumbi, vinyesi vya wanyama na baadhi ya vyakula.Uchafuzi wa mazingira kama moshi na baadhi ya harufu kali.Baadhi ya kemikali kwenye maeneo ya kazi hasa kwenye viwanda kama vya rangi, chuma, sementi na vigae.Baadhi ya wagonjwa wanaotumia dawa za kushusha shinikizo la damu zilizo katika jamii ya beta-blockers kama vile propanololwapo katika hatari ya kupata shambulio la ugonjwa wa pumu.Magonjwa kwenye mfumo wa kupumua yasabishwayo na baadhi ya virusi na bakteria kama vile rhinovirus, Chlamydia pneumonia auBordetella pertusis.Matumizi ya mapema sana ya baadhi ya dawa hasa antibiotiki kwa watoto yanaweza kubadilisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na hivyo kumfanya mtoto kuwa katika hatari ya kupata pumu.Ongezeko la msongo wa mawazo huweza kusababisha pumu na matatizo katika mfumo wa upumuajiUpasuaji wakati wa kujifungua (caesarian section):Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kujifungua kwa njia ya upasuaji huongeza uwezekano wa kupata pumu kwa vile njia hiyo yaweza kuathiri mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.Vihatarishi vya ugonjwa wa pumu 

Uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu huongezeka iwapo mtu 
Atakuwa na magonjwa ya mzio kama vile magonjwa ya ngozi (eczema) au homa isababishwayo na aina fulani ya vumbi (hay fever)Atavuta chavu (pollen) kutoka kwenye maua au mitiAtajihusisha na uvutaji sigaraAna historia ya ugonjwa wa pumu au mzio kwenye familiaUtumiaji wa dawa aina yaaspirinAna msongo wa mawazoAna uambukizi wa magonjwa ya virusi kamarhinovirusMazoeziAnaishi sehemu zenye baridiAna matatizo katika njia yake ya chakula (Gastroesophageal reflux disease au GERD)
Dalili za ugonjwa wa pumu 

Dalili za ugonjwa wa pumu ni pamoja na 
Kuishiwa na pumzi na kupumua kwa shida (shortness of breath)Kutoa sauti kama mtu anayepiga miluzi wakati wa kupumua (wheezing)Kukohoa sana (chronic cough)hasa nyakati za usiku au asubuhi. Aidha kikohozi huambatana na kutoa makohozi mazito, yasiyo na rangi au yenye rangi ya njano.Kubana kwa kifua.Kwa mtu aliyepata shambulizi kubwa la pumu (severe asthmatic attack) anaweza kushindwa kuzungumza na pia kuwa na hali kama ya kuchanganyikiwa.Vipimo na Uchunguzi 

Pamoja na daktari kutaka kufahamu historia ya mgonjwa, anaweza pia kuamua kufanya vipimo vifuatavyo ambavyo vitamsaidia kufahamu chanzo na madhara ya ugonjwa wa pumu kwa muathirika. 
Kipimo cha damu (complete blood count) msisitizo ukiwa kwenye wingi wa seli za damu aina ya eosinophils ambazo uhusika na kuwepo kwa shambulio la mzio.Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kutoa hewa nje mara baada ya kuivuta (spirometery). Aina hii ya uchunguzi hufanyika kabla ya mgonjwa kupewa dawa kwa kutumia nebulizer.Kipimo cha kuchunguza kiwango cha hewa ya oksijeni kilichopo kwenye damu ya mgonjwa (oximetry).Kipimo cha kuchunguza uwezo wa mgonjwa kupumua hewa nje wakati wa shambulizi la pumu (Peak flow meter).X-ray ya kifua kwa ajili ya kutofautisha pumu na magonjwa mengine yenye dalili za kufanana kama vile ugonjwa wa moyo (congestive heart failure), magonjwa sugu ya kuziba kwa njia za hewa (COPD kama vile chronic bronchitis na emphysema) na magonjwa mengine ya kuzaliwa kama vile cystic fibrosis.Kipimo cha mzio cha ngozi(skin allergy test) kwa ajili ya kutambua aina ya mzio inayomsababishia mgonjwa shambulizi la pumu.
Matibabu ya Pumu 

Kwa ujumla matibabu ya pumu hujumuisha kuepuka visababishi vya ugonjwa huu na matumizi ya madawa kwa walio na hali mbaya. Aidha, kwa wanaopata ugonjwa huu kwa sababu ya msongo wa mawazo hupewa ushauri nasaha kwa ajili ya 

kusaidia kutatua matatizo yanayowakabili. Vilevile inashauriwa kwa wenye tatizo hili, kuwa na dawa karibu muda wote kwa ajili ya matumizi pindi shambulizi litakapotokea. Pia inashauriwa sana kuepuka mazingira na hali za baridi ambazo 

huweza kuchochea kutokea kwa shambulio la ugonjwa huu. Matibabu ya kutumia dawa hujumuisha matumizi ya dawa za kusaidia kupunguza na kuondoa makohozi (expectorants), dawa zinazosaidia kutanua mirija ya hewa(bronchodilators), dawa za kuondoa mcharuko mwili kama vile cortisone ya drip (hasa wakati wa dharura) au nebulizer, na dawa za kuzuia 

mzio (antihistamine drugs). Hata hivyo, kuna matibabu ya ziada kulingana na hali ya mgonjwa pamoja na kundi na aina ya pumu inayomuathiri mgonjwa. Kwa wagonjwa wenye pumu ya ghafla na wenye hali mbaya (acute asthma)matibabu hujumuisha matumizi ya dawa za kutanua mirija ya hewa(bronchodilators) pamoja na kuongezewa hewa ya 

oksijeni, dawa za kutuliza mcharuko mwili (steroids) pamoja na dawa za kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (intravenous muscle relaxants). Aidha kwa vile mara nyingi shambulizi hili laweza kuwa la hatari sana, mgonjwa hulazwa 

hospitali na huongezewa hewa ya oksijeni, na kwa wagonjwa wasioweza kupumua kabisa, husaidiwa kufanya hivyo kwa kutumia mashine maalum iitwayo(mechanical ventilator). Kwa wagonjwa wenye pumu sugu, jambo la muhimu ni 

kuepuka visababishi vya pumu na kuendelea na matumizi ya dawa zinazosaidia katika kutanua mirija ya hewa. Kwa wagonjwa wanaopata mashambulzi ya mara kwa mara wanaweza kushauriwa na daktari kutumia dawa kadhaa zikiwemo zile zinazopunguza mcharuko mwili(mast cell inhibitors, inhaled steroids au oral steroids), pamoja na dawa za

kutuliza kukakamaa kwa misuli ya mwili (muscle relaxants). Aidha ni vema pia kutibiwa na kuthibiti kutokea kwa magonjwa yote yahusuyo mfumo wa hewa. Matumizi ya chanjo ya magonjwa kama influenza na pneumococcal pneumonia nayo husaidia sana katika uthibiti wa kutokea kwa pumu. Ni vema pia kuepuka matumizi ya dawa za jamii ya beta-blockers kwa wagonjwa wenye shinikizo la damu na ambao pia wana pumu.

Nini madhara ya pumu kwa mama wajawazito? 

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa takribani theluthi moja ya wajawazito wenye pumu hupata nafuu kipindi cha ujauzito, theluthi nyingine hupata matatizo kipindi hiki na theluthi iliyobakia huwa na hali ya kawaida kama kabla ya ujauzito. 

Kwa kawaida dalili za pumu hujirudia kama awali miezi mitatu baada ya kujifungua. Dalili za pumu kwa mjamzito zinaweza kuwa mbaya zaidi kuanzia wiki ya 24-36 (mwezi wa sita mpaka wa nane). Ni mara chache sana mjamzito 

anapata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. Inakisiwa kuwa, ni asilimia 10 tu ya wajawazito wenye pumu wanaopata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. Baadhi ya dawa zinazotumika wakati wa ujauzito na baada ya 

kujifungua huongeza madhara ya pumu, hivyo ni vizuri kumueleza daktari kwamba una pumu kabla ya kupewa dawa. Aidha na si vyema kunywa dawa kwa mazoea.Wanawake wenye pumu isiyoweza kuthibitiwa kipindi cha ujauzito 

hupata madhara ya kuzaa mtoto njiti (premature baby), kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, kifafa cha mimba, shinikizo la damu(Hypertension), na iwapo atapata shambulizi hatari wakati wa ujauzito mtoto anaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni. 

===================================
Ugonjwa wa Pumu ( Athma kwa watoto
===================================

Nini maana ya Pumu?

Pumu ni hali ambayo huathiri njia za hewa, njia hizi za hewa pia huitwa mirija ya kupumulia. Mirija hii huanzia kwenye njia ya hewa(trachea) hadi kwenye mapafu.

Mchakato wa kupumua kwa watoto walio wengi ni rahisi : Watoto huingiza hewa kupitia puani au mdomoni na hewa huingia kwenye njia ya hewa(trachea) na kuelekea kwenye mapafu. Lakini Kwa watoto wenye pumu, hupumua Kwa shida Kwa sababu njia ya hewa hushindwa kupitisha hewa kwa sababu ya njia yao kuwa imehathiriwa na hali ya pumu.

Shambulio la pumu (Asthma attack) ni nini?

Hii ni hali ambayo hutokea wakati njia ya hewa inapo vimba na kuwa nyembamba na inakuwa vigumu kwa hewa kuingia na kutoka kwenye mapafu. Wakati mwingine njia za hewa zinapokuwa zimevimba hutoa majimaji mfano wa makamasi, hali ambayo husababisha mchakato mzima wa mabadlishano ya hewa katika mapafu kuwa mgumu na hii hali ndo inapelekea tatizo zima la mtotoanapo patwa na pumu kushindwa kupumua vizuri.

Wakati ugonjwa huu unaanza, upumuaji kwa mtoto unaweza kuwa wa kawaida na kuonekana kama vile hakuna tatizo, Lakini kipindi ugonjwa unapoanza, unaweza kuhisi kwamba mtu anapumua kupitia kwenye mrija. Mtoto mwenye pumu anaweza kutoa mlio kama wa filimbi (anapopumua), kukohoa, na kusikia kifua kubana.

Wakati shambulio la ugonjwa wa pumu(asthma attack), hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama mtoto hatatumia dawa sahii za pumu. Baada ya kutumia dawa na kupata matibau sahii wakati wa shambulio la ugonjwa wa pumu, njia ya hewa mara nyingi hurudia hali yake ya kawaida, ingawa inaweza kuchukua muda mrefu kidogo wakati mwingine.

Pumu huwapata watu gani?

Pumu ni ugonjwa ambao huwapata watu wengi zaidi ya unavyo weza kufikiri.Karibia watoto milioni sita nchini marekani wanaumwa ugonjwa wa pumu(Hatujui hapa kwetu Tanzania ni idadi gani?).Ugonjwa wa pumu humpata mtoto mmoja hadi wawili katika kila watoto 10 kwa marekani. Hii ina maana kwamba kama una watoto 20 darasani, watoto 2-4 kati yao wanaweza kuwa na ugonjwa wa pumu. Ugonjwa wa pumu unaweza kumshika mtu katika umri wowote- kuanzia mtoto mchanga hadi mtu mzima-lakini huwashika zaidi watoto wenye umri wa kwenda shule(kuanzia miaka sita na kuendelea)

Hakuna anayejua kwa uhakika kwa nini ugonjwa huu unampata mtu mmoja na kuacha mwingine, lakini tunajua kwamba ugonjwa wa pumu unatokea ndani ya familia zetu. Hii ina maana kwamba kama mtoto ana pumu, yeye pia anaweza kuwa na mzazi, ndugu, mjomba au jamaa mwingine mwenye pumu au alikuwa na ugonjwa huu wakati bado mtoto.

Ugonjwa wa pumu unapoanza,huonyesha kama vile ni mafua,ambayo huambatana na kikohozi chenye kutoa mlio wa filimbi,lakini ugonjwa wa pumu siyo wa kuambukizwa. Huwezi kuambukizwa Kama unavyopata mafua

Ni sababbu zipi zinazopelekea Kupata shambulio la ugonjwa wa pumu (Asthma attack)?

Visababishi hutofautiana kutoka mtoto mmoja hadi mwingine. Sababu zipo nyingi.Baadhi ya watoto huwa na mzio(allergy), kwa vile vitu ambavyo huathiri njia ya hewa. Mara nyingi vitu vinavyoleta mzio kwa watoto wenye pumu ni vijidudu vidogo jamii ya mchwa vinavyopatikana kwenye vumbi, harufu mbaya (kama ulikuwa karibu na dimbwi na kuvuta harufu hiyo), mbelewele(pollen) kutoka mitini, majani na kwenye magugu.

Watoto wengi hupata shambulio la pumu wanapokuwa karibu na wanyama wenye manyoya kama Paka na mbwa,baadhi watoto wanapovuta hewa iliyochanganyika na chembechembe za manyoya hawa wanaweza pata shambulio la pumu.

Visababishi vingine ni pamoja na marashi(perfumes), vumbi la chaki, na uvutaji wa sigara. Uvutaji wa sigara sio mzuri hasa kwa mtu mwenye pumu.

Wakati mwingine maambukizi mbalimbali yanaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa wa pumu,maradhi kama mafua, Kwa baadhi ya watoto, hali ya hewa yenye baridi inaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa huo,baadhi ya watoto hupatwa na matatizo ya pumu wanapokuwa wanafanya mazoezi,hii ni aina ya pumu inayosababishwa na mazoezi.

Jinsi gani unaweza kutibu ugonjwa wa pumu kwa watoto?

Watoto wenye ugonjwa wa pumu wanatakiwa kujaribu kuepuka visababishi vyote vinavyoweza kuwasababishia shambulio la hewa.Ingawa kuna baadhi ya visababishi kama vumbi la chaki ni vigumu kuviepuka katika mzaizngira yetu hasa shuleni,lakini mtoto,wazazi na walimu wajaribu kuwasaidia watoto wenye matatizo haya.

Sura ya ugonjwa wa pumu hutofautiana kutoka kwa mtoto mmoja hadi mwingine, hivyo kuna dawa mbalimbali za kutibu ugonjwa wa pumu,na matibabu haya hutofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine hii ni baada yake daktari kujaribu kufuatilia sababu zilizopelekea ugonjwa huo, ni kwa kasi gani ugonjwa umetokea, na kiwango cha madhara ya ugonjwa huo. Hapo ndipo ataamua tiba ipi itakuwa sahii na bora kwa mtoto.

Baadhi ya watoto wanatakiwa wameze dawa za pumu mara kwa mara punde wanapopata ugonjwa huu. Hii huitwa dawa ya dharura kwa sababu hufanya kazi ya kufungua njia ya hewa ili mtu aweze kupumua. Watoto wengine wanatakiwa kutumia dawa za kudhibiti ugonjwa wa pumu kila siku,Dawa hizi huzuia shambulio la ugonjwa(asthma attack) kutokea.Kwa hiyo matibabu ya Pumu yanatofautina kutoka mtoto mmoja na mwingine.

Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.

UJUMBE WA KUPELEKA NYUMBANI:

Mzazi au mlezi anayeona mtoto mwenye dalili za ugonjwa wa pumu kama nilivyouelezea hapo juu kitu cha kwanza cha kufanya ni kumwaisha Katika kituo chochote cha Afya au Hospitali iliyo karibu nae.

Na kwa wale watoto walikwisha gundulika tayari na ugonjwa huu wa Pumu ni kuhakikisha wanafuta masharti yote ya Matibabu ili kuzuia shambulio la ugonjwa huu.

Mtoto anayejua mapema kwamba kuna vitu vinamletea madhara katika njia ya hewa au sababu nyingine anaweza kutumia dawa mapema zitakazosaidia kufanya njia ya hewa iendelee kuwa wazi.Mtoto ambaye hupata pumu anapofanya mazoezi anaweza kutumia dawa kabla ya kufanya mazoezi ili waweze kumaliza mbio au michezo vizuri.

Kwa watoto walio wengi ugonjwa wa pumu hupona au hupata nafuu wanapokua wakubwa. Baadhi ya madaktari wanadai kwamba hii hutokea kwa sababu, njia ya hewa hupanuka kadri mtoto anavyokua mkubwa. Njia ya hewa inapopanuka, hewa huingia na kutoka kiurahisi

Baadhi ya watu wazima hupata ugonjwa wa pumu, lakini hii haiwasumbui.Wanariadha wengi katika mbio za olimpiki na magwiji wengine wa michezo wanaweza kuendelea na michezo hata wanapokuwa na ugonjwa wa pumu.