Jumatatu, 27 Februari 2017

Mungu wangu hajaniacha 8

. MUNGU WANGU HAJA NIACHA 8

Ilipo ishia

@mama yule ni kichaa ee@mama akanambia shhhhhh. Kugeuka nikamuona yupo nyuma yangu na chuma kubwa. Nikaogopa ..    Akaliweka chuma hilo mlangoni kuzuia mlangu usijifunge kisha wakaanza kuslamiana na mama kwa furaha hatimae tuka tambulishwa kua ndio bibi mzaa mama huyo tukajuzwa na ndugu wengine pia

Tulianza maisha ya arusha kwa shida mama alianza kwa biashara ndogo ndogo  hatimae akazoea akapata kazi katka kampuni moja inayo Lima kahawa iliitwa MANYARA campany.. Kampuni hiyo ilijenga nyumba nyingi zakuishi wafanaya kazi mama alifanikiwa kupata kazi katika kampuni hiyo na nyumba ya kuiahi ya viumba viwili na sebule nami nikafanikiwa kupata shule

Kwaupande wangu mwanzo nlipata shida maana shule ilikua mbali sana kias cha kutembea saanzima ndo nifike shule nilikereka kwani singinda nilitembea dakika tano nakuingia shuleni.   Lakin sikua na budi nikaendelea na shule   maisha ya arusha yalikua na nafuu kidogo    hatukulipa kodi  na kazi zilikua za uhakikka kwani kaha ndio ilikua msimuwake   ilikua wafanya kazi woote mkifika mashambani mnakatiwa miraba kwajili ya kuvuna kahawa zilo iva na kuacha mbichi.  Kadri una vyo vuna ndio kipato kinaongezeka. Kwani ilihesabiwa kila ujazo was sado moja unalipwa kia NNE hapo sasa uwezo wako mama yangu aliweza mpka sado 6 na siku nilio enda kumsaidia had I sado 11 zilifika  maisha ya liendelea

Mwaka mmoja baadae.

Nikiwa darasa LA NNE  ahule ya msingi ndurumeti ninayo soma arusha walinizuia kufanya mtihani wa kuhama darasa kutoka lanne kwenda la tano       wakasema.   Wakati nakuja nilichukuliwa cheti chmda sio chamoja kwamoja        hivyo nirudi singida katka shule yangu ya awali nikafanye mtihani.  

Taarifa hizo mama alizipokea kwa unyonge sana  hakua na lakufanya kwani singida Alisha hama kabisa    nilikaa Siku kadhaa bila kwenda shule   hatimae mama akapata wazo na kuniandalia safari nirudi singida   niende hadi kwa baba

Tulikua kama watu tulo sahau yalo tokea hatuku ya waza kabisa .
Safari iliwadia nikiwa na barua yangu nlotoka NATO arusha nikaiahika madhubuti na safari ikaanza kwa tashrifu hadi singida

Singida tena kwamama wakambo

Nilifika singida jioni nakumkuta Mamdogo make wabab akiwa nyumbani alinipokea vizuri tukapiga stori za arusha  akanipa chakula nikala  akaniomba barua nlokuja nayo aihifadhi nikampa   jioni baa alirudi nikamwambia lengo    nikamwambia baba kesho ni j3 twende shule ukanikabidh nifanyw mtihadi .lakin baba hakuafiki I kwenda shule alimwachia Mamdogo jukumu hilo asubui yake
Nikajiandaa vizuri na nguo zangu za shule nikawa tayari. Kisha nikamwambia Mamdogo kitayari twende. Jibu alilo nipa @ hao wanangu wanenda shule wenywe mi nikupeleke we mkubwa mzima Nina wazimu toka usinisumbue@

Nikaogopa kwaunyonge nkamwambia @bas naomba ile barua niendee@akajibu kwa ukali @aaaaa acha kunisumbua jumanne kawabie ume poteza@ kweli bioa mafanikio ya ile barua nikaenda shule
Kweli Shule walikiri kunitambua ila walitaka barua nlotoka nayo arusha   nilirudi nyumbani nikiwa nalia sikua na sim yakumfahamisha mama yalio jiri.    Nikiwa njiani narudi nilijikuta tu natamani niache ahule sasa niwe huru na mambo yangu. Wiki zilikatika bila kwenda shule hakunonekana kunisaidia baba wala mamdogo

Taratiibu nikajikuta naicha shule.  Maishaya pale nyumbani yalini shinda maana nikitukanwa kila Mara nikipo omba chakuala Mara nyingi nilijibiwa @ sijaolewa na wanaume wawili@

Mwisho nikajikuta nayakumbula mapenz ya mama yangu namkumbuka mama yangu natamani nirudi arusha kwamama

Sikh moja usiku nilikorofishana na madogo na akanipika sana kwa kutumia mwiko nilivumilia mwishi nika shindwa nika udaka mwiko nikamwambiaaaa

Mimi simtoto wako na si ndugu yako unanipiga kama nan wako .

Maneno Yale yalimkera sana akanyanyua mwiko tena anipige kichwani nami nioanyanyua mkonooo wangu.......... .

Itaendelea sehem ya 9

Jumamosi, 25 Februari 2017

Mungu wangu hajaniacha 7

Mungu wangu hajaniacha 7

Ilipo ishia 6

nikapikaa ugali mboa zikaivaa nikapakua wa mama nikauweka chini ya meza nasisi.      tukaanza kula wakati tunakula ghafla nikaskia.......

Sasa endelea Shem ya 7

Nikaskia mlango ukigongwa kwanguvu kufungua niyule kijana alo poteza ela yake kaskia nimeipata kaifuata kwakua nilimuogopa nikampa iliopo 455 na maelezo ya kutosha akaridhika na kuondoka si tukaendelea na msosi

Jioni yake mama alipo rudi alistaajabu na kunisifia kua naweza kuwahudumia wadogo zangu hata kama yeye hayupo.    Pia mama aliongeza kua anaandaa safar ya arusha tukamsalimie bibi mzaaa mama
Jumatatu sikuenda shule mama alihangaika kutafuta uhamisho maana alitaka tukakae nikasome kule hatimae j5 ilifika tukapanda tashrif   kwamara yangu yakwanza napanda bas kubwa LA mkoa bas lili kimbia vumbi lilitawala ndani utadhani tulipishana na mifugo lakin no Barbara ndo haikujengwa majira ya SAA kumi jioni tulifika arusha mjini hapo nilimskia mama akiuliza @samahan baba hari za ngaramtoni ya juu ziko wapi@ usijali mamaaa fuata njia hiii ukifika mbele uliza kilombero@ baada ya maelekezo hayo tulitembea mama hakitaka kuuliza tena hivyo tulizungukaa badae tukaona gari ndogo haic nyingi huku kelele za makondakta zikisikika.   Usarivaa wengine ungalimited wengine ngara kila moja alitaja eneo tofauti Mara tukaona gari imeandikwa ngaramtoni ya juu tuka panda tuka kaa     gari ilianza safar gari ilisimama Mara kadhaa watu wakishuka vituo nlivyo kumbuka waloshuka watu ni sakina+kwa idy+ njiangombe+. Hatimae kibaoni hapo tulishuka  na gari ikaondoka  tukachkua bodaboda mbili tukaingia kushoto dakika tano tulishushwa mbele yanyumba ya mabati ilio ezekwa bati chini mpaka juu       hapo walio mjua mama walimpokea tukaingia katika major yanyumba hizo lakin nje karibu na jalalani palikua na bibi amesimama alituona lakin hakusogea pale alipo kama MTU alie kua katika ibada huku aliimba nyimbo ambayo binafs nilijiuliza maswali sikupata majibu muda wote nilikua nikitega skio kwani sauti ya bibi huyo ilikua tam hatimae nika inasa nyimbo aliimba hivi
@ staki madhambi staki madhambi staki madhambi# siiitaaaakiiii dhambiiii napiiiiingaaa dhaaambi taaaaakiii dhambi 'taki madhambi taki madhambi napinga  napiiiiiiingaaaa dhambi

Alirudia sana nyimbo  hiyo

Mwisho nkapata swal lakumuuliza mama

@eti mama yule pale ni kichaaa ee@  mama akanijibu shhhhh
Kugeuka nyuma nikamuona yupo nyuma yangu na chuma kubwa nikaogopaaa

Itaendelea sehem 8

Ijumaa, 17 Februari 2017

Mungu wangu hajaniacha 6

MUNGU WANGU HAJANIACHA 6

Iilipo ishia sehem ya 5

ghafla nika skia chafya nika geuka  nika kutizama usoni nikaskia tena chafya kutoka katika kinywa chako ukaananza na kukoroma hapo watu wooote na madocta wakaanzaaa

Itaendeleaa sehem 6

Kushangaa kwani waliamini tayari ushakuafa    nikajikuta napata ujasisiri wahali ya juu na ghafla nika nyanyuka na kuju tizama @haya mama una bahati sogea sasa@ alisema docta mmoja nami kwa ujasiri nikamjibu@tafadhali niachieni ntawaita @hapo madocta bila kujibu wakondoka
Nilipo kutizama ndipo nika gundu kuna kitu unataka kukitapika lakin kinarudi ndani hapo nika chukua kanga yangu ni kaiviringisha mfano wakamba nikaingisha kinywani mwako hadi kwenye koo nilipo vuta ilitika na mlenda lakin ukiwa na ranging nyeusi kama ya mkaaa nika rudisha tena hapo nikatoa tenalend mweusi wakati huu ulikua watoka kama kamba ilio tumbukia tumboni nilifanya Kai hiyo kwa dakika zaidi ya 20 muda hakuna kicho toka nikaami ghasia zoote zatumboni nsha zitoa.  Kwambali nikaona mwili wako una pata moto nilipo weka mkono kifuani kwako nikagundua mapigo ya moyo tana piga kwa kasi  hapo nikaita @doctaaaaaaaa@sauti haikua kubwa lakin watu walio nisikia walinisaidia kuita muda tu madocta wakafika walipo kuti zama ana kukushishika hapo nikaskia docta akisema @leteni drip LA maji @kauli hiyo ikinipa moyo sana naada ya kutundukiwa drip ya maji docta mmoja akasema kwasauti @jamani kuam bina damu wanaroho mbaya sana ni sawa na wachawi@ kisha akanigeukia mimi nakunambia @mama usimuache mungu wako maana AME kusaidia @nami nikamkijibu   @nikweki docta nakiri namimi kua. MUNGU WANGU HAJA NIACHA. Amekua nami nandio kawa rafiki wakweli kwangu kanipa moyo watu  walipo nikatisha tamaa

Baada ya hapo ulikaa Sikh tatu bila faham hatimae uka pata faham alhamdu lillahi

Mama ali maliza stori kwa upande wake  hapo nikaelew kwanini mi nilikua hospitali
Ila katila kumbu kumbu zangu nilikumbuka sana mda mchache kabla ya hali ile kutokea kua chanzo ni mboga ya mchuzi wanyama nilio imba sasa picha yote ya ubaya wa mama mdogi ilinijia usoni machozi ya litiririka

Mwaka mmoja baadae

Nilikua darasa LA tatu dhiki shida nataabu zilituandama baba hakua na msaada wowote kwetu mama alijihangaikia mwenyewe kwa biasharandogo ndogo sokoni wakati mwingine sikuenda shule nikamsaidia mama biashara niliuza ndizi viazi asubui hatula chochote macha na na na usiku tulijunywa uji pesa ilikua ngumu kupata japo ilikua na thamani maana kipindi hiko ilikua ni awamu ya pili ya utawala wa mwinyi

Nakumbuka sikumosh 

Ikilikua j pili.  Majira ya SAA name mchana nikiwa nyumbani njaa inauma wadogo zangu wamelala kW uchovu was njaa nikaamua kutoka nje na kutembea tembea nikapoita nje katka nyumba moja jirani anako ish nwanafunz mwenzangni nikaona mabox mawili makubwa ya TV yametupwa jalalani nilipo kaza macho   katika box moja lililo kua wazi nikaona karatas nililo his kua ni hela nikasoge nakulichukua naaam ilIkua ni sh 1000 elf moja yakaratasi hapo. Moyo ukaenda mbio nika ichukua sikujiuliza nikaanza mbio had I nyumbani nipo fika nikamkuta mdogo wangu wakiume Amalia nikauliza mini nkaambiw njaa nami kwaujasir nkawaambia @subirini nakuja sasa iv na BONGE LA saprais@hapo nikaondoka hadi katika duka LA shayo shop niaanza kuagiza 


@shayo nipe Unga dona kilo moja sh 75 sabini Nagano NAFTA ya mboga kijiko kimoja 25ishirini na tano mafta ya taa yakuwashia moto ya 30 thelathini kiberiti kimoja sh 15 kumi Natano

Kisha nikalipa nikasigea kibandani kwa mama shayo nako nika nunua dagaa was sh150 mia na hamsini nyanya na vitunguu vya mia 

Hapo jumla nkawa nimetumia sh 295 miambili na tisini na tano nikabakiwa na  sh705 nika lipa deni alokua akidaiwa mama LA sh mia nikabakiwa na 605 nikanunua mkaa was miana hamasini150 ikabaki 455 nikaenda nyumbani nikapikaa ugali mbiga zikaivaa nikapakua was mama nikauweka chini ya meza nas tukaanza kula wakati tunakula ghafla nikaskia...


Itaendelea sehem ya 7

Mungu wangu haja niacha 5

. MUNGU WANGUHAJA NIACHA 5

Ilipo ishia sehemnya 4

mbele yangu ni kamuona jirani wa baba yako nika muuliza @mama neema kime mkuta mwangu@ akanivuta pembeni na kuanza kuniambia

Itaendelea sehem ya 5






Sasa endelea

Mwanao alipo toka shule akaingia ndani sisi hatujui kilicho endelea ndani  muda tu mama yake mdogo alitoka haikupita mda tukaskia MTU ana koroma ndani tukaogopa tulipo ingia tukamkuta Jumanne akitupa miguu na mikono povu lime mjaa mdomoni    sisi tulikua wanawake watupu tuka sh indwa kumsaidia ikabidi tuwaite vijana wakambeba na kumleta hospitali hayo ndo nnay yajua. Alisema mama neema @ hapo nikawaza nini chakufanya nikarudi wodini nikakutizama akili iianijia tu ntoke nkatafute maziwa .wakati natoka mama hamza (mama yako mkubwa yan Dada yangu) nae akaja nikamuagiza naziwa lakini sikuweza kumsubiri nami nkatoka iilikua nikaz kuyapata lakin nika fanikiwa  nikaja haraka na kuku nywesha japo meno yalikua ya me umana lakin nilifanikiwa kuya achanisha hatimae maziwa yakapata nafas yaliingia kama mahi yanavyo ingia mtungini nusu Lita ikaisha hakuna dalili yeyote nakir sikujua kwanini nakupa maziwa na sijui nilitarajia nini ilikua ni roho fulan iko ni sukuma   wakati nime KATA tamaa maana maziwa yameisha bila dalili yetote jicho bado jeupe mapigo yamoyi yamesimama mwili umeka baridi machozi yalikua yakinibubujika kama bomba zamaji wagonjwa na walio ni tizama walisikika maskioni mwangu wakisema @mwachen kachanganyikiwa na mwanae aki thibitisha kua kafa au waiteni ma docta waupeleke mwili mochwari @ hapo nikashtuka nilipo skia mochwari nikaogopa Mara Dada nae akafika na maziwa nlo muagiza nikayachukua bila neno nika kunyweshaa yoote bila kubaki Mara madocta nao wakafika @mama tafadhali huyo kesha kufa hatakiwi kuwapo hapo @ ghalfla nikapata ujasiri hasa nilipo kumbuka kua mafundisho ya din yanasema pale unapo kufa INA maanisha na rizki zako ya dunuani Imeisha bas hata upewe nin hakito pita kinywani ...kumbukumbu hizo zikinifanya niamin mwanagu hajafa mbona maziwa Lita nzima imeingia mwilini mwake inamana bado you hai wakati nataka kusema neno na sijui nilitaka kusema nini mbele ya madocta
ghafla nika skia chafya nika geuka  nika kutizama usoni nikaskia tena chafya kutoka katika kinywa chako ukaananza na kukoroma hapo watu wooote na madocta wakaanzaaa

Itaendeleaa sehem 6

Jumatano, 15 Februari 2017

UFAHAMU +UMOJA WAWA HADHIRI WAKIISLAM TANZANIA

UMOJA WAWAHADHIRIbWAKISLAM TANZANIA
Kwaufupi (UWAKTA)

Nitaasisi yakislam ilio anzishwa na wahadhiri wakiislam watanzania

Ndugu mwislam
Tukirudi nyuma kifikra tuka kumbuka kua asilimia kubwa ya wale mashekh walio tupa mwanga wa kazi hii ya kufanya mihadhara wengi wao washa tangulia mbele za haq
(Allah awarehemu huko waliko)

Kazi ikabaki Nikonini mwa wale walio jifunza zani na sasa
Kazi hii ilifaana sana kutoka ilipo anzishwa mpaka miaka ya 2005

Ambapo kazi hii ilianza kupata misukosuko ya wazi kama kukamatwa kwa wahadhiri na kutiwa ndani kunyimwa vibali na k:

TUKUMBUKE FAIDA ZA MIHADHARA ambayo asili yake ni vitabu vinne (torat zaburi injili na qur.an)

Ilifanya vazi LA kanzu kuheshimiwa mpaka sasa nikawaida kumuona MTU akiwa ofisini na kanzu na kofia

Mtiririko was waislam wanao ritadi kwakuuacha uislam kwa miujiza au msaada pia ulipungua kutokana na na ukweli ulio simamiwa na wahadhiri
Nihayo na mengine mengi ambayo mihadhara ya kiislam ilikua ni sababu ya kufahamika

KUPUNGUA KWA NIHADHARA
YA VITABU VINNE KWASASA

Hii INA sababishwa na mabadiliko ya utendaji wamihadhara hiyo wahadhir wengi sasa kufanya mihadhara inayo wahusu waislam tu kiitikadi hivyo kupungua ufanisi wamihadhara ya vitabu vinne   walimu wamihadhara hiyo kutoweka dunian wakati vijana wano takiwa kujifunza mijadala hiyo wakowa bize a maslahi ya dunia tu

KUTIZAMWA TOFAUTI KWA WAHADHIRI NAWAISLAM

Hali ya zamani na sasa nitofaut kwa wahadhir wakiislam. Zamani wahadhiri walikubalika mbelebya waislam waliitwa mahala wanapo hitajika walichangiwa gharama za uendeshaji mikutani bila lawama waliheshimika mahala walipo onekana  heshma yao ilikuwa kubwa matamko yao yaliheshimiwa na waislam Tanzania. Waliaminiwa nakusikilizwa kila mahala mihadhara ya wahadhiri ilijaa watu kwa matangazo machache tu wakati mwingine matanagazo hayakufanyika lakin watu walijaa viwanjani

LEO HII

Wahadhiri wengi wajazaraulika ispokua wachache. Mihadhara ili iwe na watu wengi matangazo yafanyike sana magari ya pite vipeperushi na na hata vipindi vya redio na TV pia matangazo ya dizainiwe ili ya waguse watu. Wakati zamani walipo sema kutakuana kuhadhara maeneo Fulani wahadhiri fulani watakuepo ili tosha  ni tofauti na sasa   
Imefikia wakati ukijulikana wewe ni mhadhiri nafas msikitini hupewi

Baada yawa hadhiri wanao jitambua kulitizama hili wakagundua

Baadhi ya watu hukurupuka kufanya mihadhara jali hawana elimunayo

Pia watu wanaharibu mazingira ya dini kwa nembi ya uhadhiri

Wengine kukosa kujua kanuni za kazi hiii hivyo kuifanya kimakosa
Pia kutoweka kwa ikhlaswi kwa wahubiri wengi

NDIPO

Wahadhiri wakiislam wakaamua kuanzisha taasisi hii ya (UWAKTA))

Lengo

Ni kurejesha hadhi ya uislam kupitia mihadhara

Kurejesha hadhi ya mihadhara ya kiislam

Kudhibiti wanao haribu dini kwa nembo ya uhadhiri
Kuwadhibiti hata wahadhiri wano haribu kwa  kua na Uhuru ulo pitiliza

Pia kuhakikisha waislam wana pata faida zitokanazo na mihadhara na wahadhiri

Iki lengi lingine LA taasisi hii ni

Kuandaa miradi itakayo saidia kujenga shule na vyuo vyakielimu

Hospitali kwajili ya tiba  zakisheria

Ajira kwa vijana na wazee

Ili kukamilisha hayo

Taasisi ya Umoja
Ikiongozwa na viongozi mahiri

Pamoja na amiir shekh raajabu juma alqushairiya

Ina utaratibu

Wakusajili wahadhiri woote Tanzania na nyadhifa zaobna aina ya harakati zao

Nakutoa vitambulisho kwa wahadhiri hao 

Hii itasaidi kufaham nchi yetu ina wahadhir wangapi

Pia akipata tatizo mmoja wetu kufaham kiurahisi

Na kusaidiana pia

Umoja itashirikiana na taasisi zingine zakiislam kukamilisha malengo


Hii nisehem ya kwanza inayo uhusu Umoja wawahadhir wakiislam Tanzania

Utazidi kupata taarifa zaidi inshaallah

Tafadhali toa maoni yako hapa chini  juu  ya namna ulivyo elewa



Ijumaa, 10 Februari 2017

الاستاذ هد هد(kuhusu VALENTINE DAY) NAUISLAM

. HISTORIA YA SHEREHE ZA SIKU YA VALENTINE

  

   Asili yake ni sherehe ya kipagani iliyoanzia mjini Rome Italy.Ikaingia kuwa ya kidini na sasa imekuwa ikitumika kama ni msimu wa kufanya biashara huria ambapo biashara za vyakula na mapambo ya maua, dhahabu na vyakula kama chakleti huchangamka sana.

  Warumi wa kale walisherehekea siku za tarehe 13,14 na 15 kwa matambiko mbali mbali yenye lengo la kutafuta uzazi kwa jina la siku ya Lupercalia.Wanyama wa kila aina walichinjwa ambapo vijana wa kiume walijitapakaza damu zao na kubeba mikia ya wanyama hao huku wakiwa uchi na kufukuzana na wasichana huku wakiwapiga migongoni kwa lengo na kukuza urutuba wa uzazi.Warumi hao waliamini kuwa muasisi wa mji wa Rome anayeitwa Romulus siku moja alinyonyeshwa na mbwa mwitu na ndipo akawa mwenye hekima na shujaa.

  Ukristo ulipoingia Rome pole pole sherehe hizi ziliingia ndani ya mafundisho ya dini.Kwa mfano yapo masimulizi kwamba Valentine alikuwa ni kasisi (bishop) mnamo mwaka 197 A.D wa mji wa Interamna ujulikanao sasa kama Terni.Kasisi huyo aliuliwa na viongozi wa kijamii baada muda mfupi kutokana na imani yake ya kikristo.Inaaminika alikufa siku ya Februari 14.

  Kisa kingine kinamtaja kasisi mwengine wa mji wa Rome kwa jina la Valentine ambaye naye inaaminika aliuwawa Februari 14.Kosa lake la mwanzo linatajwa kwamba  akiwa jela aliweza kumponya upofu  motto wa afisa gereza ambaye baadaye akafanya mahusiano naye ya kimapenzi.Alikuwa akiandikiana barua naye kwa kutumia damu yake kama wino.Hiyo barua ikiweka saini yake kama  “From your Valentine”.Kisa kingine cha kufungwa kwake inasemekana mtawala wa Rome wa wakati huo Claudius alikuwa amekataza wavulana kuoa ili awe na askari wazuri.Kasisi Valentine aligundulika kufungisha ndoa kwa siri ikabidi akamatwe.

   Mnamo mwaka 496 A.D papa wa wakati huo Gelasius kwa kuvutiwa na wimbi la sherehe za siku ya Valentine akaamua kwamba kila Februari 14 iwe ni siku ya sherehe ya kikristo kwa ajili ya kumuadhimisha St.Valentine.

   Kuifanya Februari 14 kama siku ya wapendanao kulipata nguvu zaidi mwaka 1382 wakati  Richard П wa London alipotangaza uchumba na Anne wa Bohemia.Richard aliandika   “For this was on St. Valentine's Day/ When every fowl cometh there to choose his mate.”.

   Mwaka 1400 A.D mahakama maalum ilifunguliwa  siku ya Valentine kushughulika na kesi mbali za mambo ya mapenzi kuhusiana na wachumba kupigana,kuachana na mateso mengine ya kimapenzi.

 Kufikia mwaka 1601 sherehe za Valentine zilikuwa zimezoeleka sana katika maisha ya kawaida kiasi kwamba  William Shakespeare aliandika katika shairi lake

 “To-morrow is Saint Valentine's day,/All in the morning betime,/And I a maid at your window,/To be your Valentine.”.

 

  

  Utaratibu wa  kutumiana kadi za mapenzi ulianza rasmi mwaka 1847 jijini London wakati shughuli za uchapishaji ziliporahisika.Mwaka 1929  kwa mara nyengine sherehe za Valentine zilileta janga kubwa pale magenge matano  jijini Chicago,Marekani  yalipopigana na kuuana kwa risasi  kuhusiana na mambo ya mapenzi.

    Katikati ya ya miaka ya 1980 makampuni  ya madini na biashara nyenginezo  yalianza kuziteka nyara sherehe za Valentine kwa  kuhamasisha  watu kununua bidhaa zao.

 

     Kutokana na historia hii itaonekana kwamba  sherehe zaValentine Day  hazina uhusiano wowote na uislamu.  Allaah سبحانه وتعالى   anasema:

((وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))

((Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasirika)) [Al-'Imraan:85]

 Mtume  صلى الله عليه وآله وسلمametuambia kuwa kutakua na makundi katika ummah wake ambao watawafuata maadui wa Allaah سبحانه وتعالى  katika desturi na mila zao kama ifuatavyo:

((ستتبعون سنن من كان قبلكم شبراً بشبر وذراعاً بذراع حتى لو دخلوا جحر ضب لدخلتموه)) قالوا: أتراهم اليهود والنصارى؟ قال: ((فمن إذن؟)) البخاري ومسلم

((Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika hadi wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia)) Wakasema (Maswahaba): Ewe Mtume! Je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: ((Hivyo nani basi mwengine?)) Al-Bukhariy na Muslim

Jumatano, 8 Februari 2017

UMOJA WA WAHADHIRI WAKIISLAM TANZANIA (UWAKTA)

. . السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Umoja wawahadhiri wakiislam tanzania
(UWAKTA)

Una waalika waislam wote katika kongamano la kumbu kumbu na dua juu ya ma shujaa wana harakati wa da.wa na tukio la mwembe chai  lililo ibua historia  kubwa katika harakati za dini tukufu ya uislam nchini

Lengo la kongamano hilo

Ni kuwakumbuka mashujaa walio husika katika tukio lamwembe chai nakuwaombea dua mashekh wetu walio tangulia mbele za haq   

Pia kuzungumzia qadhia ya mashekh na wanaharakani walioko matesoni magerezani na kwingineko

Shime alayku wailam  tuhudhurie kwawingi

Kongamano lita fanyila
Tare 12 mwezi wa 2 mwaka huu 2017
Itakua siku ya juma pili. Litafanyikia
Msikiti wa mwembe chai TIC

Wageni kutokanchi za jirani wataanza kupokelewa j mos

Pia wahadhir wakubwa wahapa nchini  watakuwepo 
Na uongozi mzima wa Umoja wawahadhiri wakiislam Tanzania (uwakta)

Nyooote mna karibishwa


Share na wengine wapate taarifa hii sambaza katika mitandao ya kijamii